BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BREIVIK ALIYEUA WATU 76 NORWAY ALILENGA NA SEHEMU NYINGINE PIA.


Polisi wa Norway wamethibitisha kuwa Anders Behring Breivik, ambaye amekiri kuuwa watu 76 juma lilopita alikuwa akifikiria malengo mengine pia.

Mazishi ya Bano Rashid aliyeuliwa na Breivik yamefanywa kwenyE kanisa mjini Oslo watu 69 waliuwawa katika kisiwa cha Utoeya na 8 kwenye mripuko wa bomu lilotegwa kwenye gari kati ya mji wa Oslo mapema siku hiyo hiyo.

Msemaji wa polisi, Paal-Fredrik Hjort Kraby, alieleza kuwa alipohojiwa, Breivik alizungumza kwa jumla kwamba alikuwa na malengo mengine pia.

Lakini msemaji huyo alikataa kuthibitisha tetesi kwenye vyombo vya habari kwamba kati ya malengo hayo mojawapo ni kasri la kifalme na makao makuu ya chama tawala cha Labour.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: