BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Teknolojia katika soka


Teknolojia ya kutumia kamera katika goli huenda ikaanza kutumika katika ligi kuu ya Premier mwanzoni mwa msimu ujao wa 2012-13.
PICHA YA MPIRA IKIONYESHA UMEVUKA MSTARI WA LANGO ENEO LA GOLIKIPA NA KUASHIRIA BAO HALALI AMBAPO MIPIRA YA NAMANA HIYO IMEKUWA IKILETA UTATA AIDHA KWA MLINZI AU GOLIKIPA KUUONDOA MPIRA KWA HARAKA KATIKA ENEO HILO WAKATI HUO REFA AMBAYE NDIYE ANAYEIDHINI BAO ANAKUWA YUKO MBALI ENEO HILO NA UPENDE WA WACHEZAJI WA TIMU PINZANIA KUANZA KULALAMIKA KWA LENGO LA KUMSHAWISHI REFA KUKUBALI BAO HILO.

Halmashauri ya kimataifa ya chama cha mpira cha England itatoa uamuzi kama idhinishe mfumo huo ama la mnamo mwezi wa Machi 2012.

Ikiwa itathibitishwa basi kiongozi wa FIFA Sepp Blatter alisema kuwa ligi za soka zitaweza kuutumia mwanzoni mwa msimu wa 2012-13 endapo utakua hauna kasoro wala hautagharimu fedha nyingi.

Mkuu wa ligi ya Premier ya England, Richard Scudamore alisema watautumia mfumo huo mara tu utakapoidhinishwa FIFA lengo likiwa kuondoa utata unaojitokeza baada ya mpira kuvuka mstari wa lango na mpira kuvudi uwanjani hivyo kwa namna moja au teknolojia hiyo itaondoa utata huo.

Blatter aliongeza kusema kwamba teknolojia hiyo inaweza pia kutumika katika michuano ijayo ya kombe la dunia la mwaka 2014 nchini Brazil .

Kwa miaka mingi mkuu huyo wa Fifa amekua akipinga matumizi ya teknolojia katika eneo la goli lakini inaelekea alibadili mawazo yake baada ya mabishano makali kuzuka mnamo mwaka 2010.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: