BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KUMI WAFARIKI DUNIA KATIKA SHAMBULIZI INDIA


Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh

KUNDI la watu kumi waliokuwa na bunduki, walifanya mashambulizi ambayo ndiyo mabaya kabisa katika historia ya nchi hiyo. Sherehe mbali mbali zimepangwa ikiwemo, gwaride la polisi kuonyesha ishara ya nguvu za vikosi vya usalama, huku India ikiwakumbuka watu 166 waliouawa katika shambulizi hilo.
Ni shambulizi lililozidisha zaidi mgogoro kati ya majirani wawili Pakistan na India- hasa ilipobainika kundi linaloitwa Lashkar e Taiba lenye makao yake Pakistan ndilo lililopanga uvamizi mjini Mumbai.

Na huku India leo, ikikumbuka- wanaendelea kuiwekea mbinyo serikali ya Pakistan kukabiliana na makundi yenye siasa kali humo, kwa kile wengi wanasema Pakistan imeregea katika kuangamiza vitisho vya makundi hayo.

Mtaalamu wa maswala ya usalama kutoka India, Waslekar Sundeep anasema

'' Utawala wa Pakistan kwa muda mrefu umekuwa ukiuunga mkono kwa siri ukishirikiana makundi ya kigaidi nchini humo. Na pia wana maslahi yao- na maslahi yao ni kujenga sura ya wasiwasi. Kwa sababu ugaidi kwa ujumla huwa ni kuzusha machafuko.''

Polisi nchini India wanashika doria katika mji wote wa Mumbai, huku wakionyesha zana zao za kisasa- ishara kwamba wako imara kwa lolote. Wabunge, na wachezaji cricket pia walijumuika na raia wengine nchini India kuweka mashada ya maua na kujumuika katika maombi kuwakumbuka watu 166 waliouawa katika shambulizi hilo.

Mishumaa iliwashwa katika Sinagogi moja ya Mumbai. Viongozi wa kidini, wanadiplomasia wa kimataifa waliungana na raia wa India, katika makumbusho hayo, wakitoa mwito wao amani na umoja katika kupigana na kuangamiza makundi ya kigaidi kote duniani.

Akiwa ziarani nchini Marekani, Waziri mkuu wa India Manmohan Waziri Mkuu wa India Manmohan SinghBildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh Singh aliitolea changamoto serikali ya Pakistan kufanya kila juhudi kuonyesha mkono wake wa sheria una nguvu, dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya kigaidi nchini humo, ambao bado huru kutekeleza mashambulizi katika eneo hilo.

Mwaka mmoja uliopita magaidi kumi waliuvamia mji wa Mumbai, katika shambulizi lililoitikisa nchi hiyo na kuushtua ulimwengu mzima. Ulimwengu mzima ulibakia mdomo wazi, pale picha za shambulizi hilo lililodumu kwa siku tatu, zilipeperushwa moja kwa moja katika televisheni kote duniani.

Kati ya washambulizi wote kumi ni mmoja tu ndiye aliyebaki hai, raia wa Pakistan ambaye tayari ameshtakiwa kwa mauaji. Jana mahakama ya kupambana na ugaidi nchini Pakistan iliwafungulia mashtaka watu sita kwa kuhusika na mashambulizi ya Mumbai. Wote lakini walikanusha mashtaka hayo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: