
CHARELS N'ZOGBIA KULIA MOJA YA MICHEZO YAKE YA LIGI KUU.
Meneja mpya wa Aston Villa Alex McLeish anamuhitaji sana N'Zogbia ili azibe pengo litakaloachwa na Stewart Downing, ambaye yupo katika mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Liverpool baada ya klabu hizo mbili kukubalia dau siku ya Jumanne.
Villa pia imo katika kujiimarisha baada ya mshambuliaji wake wa pembeni na wa kutegemewa Ashley Young kujiunga na Manchester United mapema msimu huu.
N'Zogbia, mwenye umri wa miaka 25, ameshacheza michezo soka ya England mara 250 akiwa na klabu ya Wigan pamoja na klabu yake ya zamani ya Newcastle.
0 comments:
Post a Comment