BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MCHEZA WA KIUNGO BOMBOM SPORT CLUB KUFANYA MAJARIBIO KLABU YA AJAX CAPE TOWN YA AFRIKA YA KUSINI JULAI 25 MWAKA HUU.


Kiungo mchezeshaji wa timu ya soka ya Bombom ya jijini Dar es Salaam Shabaan Mohamedi (VESO) kushoto akimiliki mpira huku mlinzi wa timu ya Villa Squid Abdul Nassoro kulia akipiga mahesabu ya kumdhibiti wakati wa mchezo wa fainali kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 katika mashindano ya Moro Youth Cup 2011 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ambapo Villa Squid ilishinda kwa penalti 4-3 baada ya kumalizika kwa dakika za kawaida kwa kutoa suluhu ya 0-0.


MCHEZAJI wa kiungo wa kati, Shabaan Mohamedi (16) wa timu ya soka ya kituo cha michezo cha Bombom Sport Club cha Jijini Dar es Salaam anatarajia kuondoa nchini julai 25 mwaka huu kuelekea nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio ya kuchezo soka la kulipwa katika klabu ya Ajax Cape Town ya nchini humo.

Akizngumza na mwanaspoti mkoani Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri Mkuu wa kituo cha michezo cha michezo cha Bombom Ahmed Kibonge alisema mchezaji huyo anatarajia kuondoka nchini julai 25 mwaka huu kwenda Afrika ya Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio kwenye timu ya vijana ya klabu ya Ajax Cape Town inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo.

Kibonge alisema kuwa mchezaji huyo ambaye anamudu vema nafasi nne katika safu ya ushambuliaji ataondoka naye kwenda nchini humo ambapo ataanzia majaribio yake katika timu ya vijana ya klabu hiyo na mipango yote ya safari hiyo yanakwenda vizuri.

Naye Shabaan Mohamedi maarufu kama Veso alisema kuwa kwa sasa amekuwa akifanya mazoezi makali kwa ajili ya kujiweka tayari kwa safari hiyo kutokana na programu aliyopewa na mwalimu wake huyo Ahmed Kibonge kufanya mazoezi asubuhi na jioni.

Mohamedi alisema kuwa lengo alilojiwekea ni kuchezea timu ya wakubwa endapo atafuzu majaribio hayo na hiyo itakuwa njia ya yeye kuelekea kuchezo soka katika bara ulaya ili baadaye na yeye aweze kutoa mchango kwenye timu ya taifa lake la Tanzania Taifa Saters.

Kijana huyo ambaye alionyesha kiwango cha juu katika nafasi ya kiungo wakati wa mashindano yaliyoandaliwa na taasisi ya Morogoro Youth And Woman Soccer Development Center (MORO YOUTH) na kuisaidia timu yake kucheza fainali chini ya vijana wenye umri wa 17 kabla ya kufungwa na Villa Squid kwa changamoto ya mikwaju ya penalti ya bao 4-3 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana kwenye mashindano hayo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: