Timu moja ya soka ya kijiji huko nchini Uingereza imepata umaarufu wa kuwa timu mbovu zaidi labda hata duniani kote baada ya kutandikwa mabao 227 katika mechi zake kumi na moja iliyocheza.
Gazeti la Metro limesema licha ya timu hiyo kufungwa mabao 55-0 katika mchezo mmoja wachezaji wa klabu hiyo ijulikanayo kama Madron FC wana ari na moyo wa kusakata soka.
Katika mchezo huo waliobugizwa mabao 55-0 wachezaji saba tu ndiyo waliofika katika uwanjani na sheria za soka zinaruhusu wachezaji waho kucheza mchezo huku kipa hakuwezakutokea katiki mchezo huo jambo lililowalazimu kucheza bila golikipa.
Meneja wa kikosi hicho chenye ari kubwa Alan Davenport ambaye anashikilia wadhifa huo kwa muda alisema kuwa inawezekana kuwa timu yake ndio mbovu zaidi Uingereza lakini amewapongeza sana wachezaji wake kwa kujitokeza.
Aidha meneja huyo katika mahojiano na gazeti la Cornish Guardian alisema timu yake itaendelea kupambana licha ya kuonyesha kiwango kibovu kwenye michezo yake.
"Timu hushuka daraja kila wakati lakini sisi hatujawahi kukosa mchezo hata mmoja tutaendelea na huu ni wakati mgumu kwentu lakini sio sababu ya sisi kuacha kucheza soka." alisema kocha Alan.
Licha ya timu hiyo kufanikiwa kupata magoli mawili katika mechi zake hizo 10 bado habari zake zimegonga vichwa vya habari katika kona zote za Uingereza.
Hata hivyo cha kushangaza ni kuwa timu hiyo sio ya mwisho katika msimamo wa ligi ya daraja la pili ya Cornish Mining League kwani kuna timu iitwayo Storm FC ndio inayoburuza mkia baada ya kunyanganywa pointi kutokana na kutotokea kucheza moja ya mechi za ligi hiyo na timu ya Madron FC ina maskani yake karibu na Penzance kusini magharibi mwa England.
Kwa hiyo usiumie sana roho kama wewe ni shabiki wa Manchester United, ambayo ilifungwa vigoli vinne juzujuzi na West Ham, au wapenzi wa Real Madrid, waliofungwa kwa taabu vigoli vitano tu na Barcelona, au Harambee stars...
Ukisikia uchungu wewe kumbuka Madron FC 55-0.
Na historia iliyowekwa na nchini ya Qatar ndio taifa dogo zaidi kuwahi kupewa nafasi ya kuandaa michuano ya Kombe la Dunia.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / VITIMBWI VYA SOKA DUNIANI TIMU YA DARALA PILI YATANDIKWA BAO 227 KATIKA MICHEZO 10.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment