PEMBE ZA NDOVU KENYA ZACHOMWA MOTO.
Kilo 700 za pembe za ndovu zakamatwa Kenya
Maafisa wa serikali ya Kenya wamekamata kilo 700 za pembe za ndovu zenye thamani ya mamilioni ya dola, wakati walipovamia uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi nyakati za usiku.
Shirika la wanyamapori la Kenya limesema kiwango cha pembe za ndovu chenye thamani kama hiyo kilikamatwa katika mji mkuu wa Addis Ababa, Ethiopia.
Shehena zote hizo mbili zikiwa na thamani ya dola milioni 10, inaaminika zilikuwa zikielekea Thailand.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi Will Ross, amesema ujangili unaongezeka kutokana na pembe hizo kuwa na soko kubwa bara Asia.
Mwandishi wa BBC amesema hata hivyo haijafahamika iwapo pembe hizo zilizokamatwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta zilikuwa zikitoka sehemu nyingine ya Afrika au zilikuwa ni za Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment