Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa inapinga hatua za kijeshi za Shirika la Kijeshi la NATO huko nchini Libya.
Akitoa msimamo huo, Bernard Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania alisema kwamba nchi yake haioni kama hatua za kijeshi ni ufumbuzi mwafaka wa mgogoro wa kisiasa nchini Libya.
Waziri Membe alibainisha kuwa Tanzania inasisitiza msimamo wake wa kutokubaliana na mashambulizi yanayofanywa na majeshi ya Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO dhidi ya Libya yenye lengo la kumng'oa madarakani kiongozi wa nchi hiyo, Kanali Muammar Gaddafi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania alisisitiza kuwa Afrika inaamini kwamba amani ya kudumu nchini Libya haiwezi kupatikana kwa nguvu za kijeshi na kwamba msimamo huo ulisisitizwa na viongozi wa Afrika katika mkutano wao wa 17 uliofanyika Malabo, Equatorial Guinea mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment