BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAASI LIBYA WATANGAZA KIFO CHA ABDEL FATTAH YOUNES.


Abdel Fattah Younes alimuasi Gaddafi na kujiunga na waasi.

KIONGOZI WA BARAZA LA MPITO LA LIBYA, MUSTAFA ABDUL-JALAL ALISEMA KUWA JENERALI ABDEL FATTAH YOUNES AMEUWAWA NA WATU WANAOMUUNGA MKONO KANALI MUAMAL GADAFF NA KIONGOZI NA KIONGOZI WA WATU HAO TAYARI AMEKAMATWA.

Alisema Jenerali Younes aliitwa kwenye mkutano ambapo alitakiwa aeleze kuhusu harakati za kijeshi, lakini aliuawa kabla ya kufika kwenye kikao hicho.

Taarifa zilisema kuwa Jenerali Younes alishukiwa kuwa na uhusiano na majeshi yanayomuunga mkono Gaddafi.

Jenerali Younes ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani ambaye alikimbia na kujiunga na upande wa upinzani mwezi Februari.

Wasaidizi wawili wa Jenerali Younes, Kanali Muhammad Khamis na Nasir al-Madhkur, pia waliuawa kwenye shambulio hilo, Bwana Jalil alisema.

Taarifa ambazo hazikuweza kuthibitishwa zilisema kuwa Jenerali Younes na wasaidizi wake wawili walikamatwa mapema siku ya Alhamisi katika eneo la kaskazini mwa Libya.

Mapema siku ya Alhamisi, waasi walisema kuwa wameteka mji muhimu wa Ghazaya karibu na mpaka wa Tunisia, baada ya makabiliano makali na vikosi vya Kanali Gaddafi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: