WABONGO TUIGE NA HILI, NA HII SISI TUITE UZINDUZI WA GEREZA KABLA YA KUFUNGWA WAFUNGWA.
Gereza moja nchini marekani mwishoni mwa wiki liliwatoza fedha watu kwa kulala ndani ya gereza.
Hiyo ilikuwa kwa watu waliokuwa wakitaka kujaribu maisha ya gerezani jipya la Cole County kabla ya wafungwa kufungwa katika gereza hilo.
iliwalazimu watu hao kulima ghalama ya dola 30 kwa kulala usiku mmoja ambao walionja maisha ya jela siku ya Ijumaa na Jumamosi.
Maafisa wa gereza hilo walisema kuwa nafasi hiyo imetolewa kwa wananchi 170 ili kulijaribu gereza hilo jipya na kupata usingizi wa jela kabla halijaanza kazi rasmi ya kuwafungia wahalifu.
baadhi ya wananchi waliolala katika gereza hilo ni pamoja na mawakili na wanandoa waliokuwa wakiadhimisha miaka yao ya ndoa.
Watu hao walipitia misingi ya kuswekwa gerezani, ikiwa ni pamoja na kukaguliwa, kunyanganywa simu za mkononi, mikanda pamoja na vito walivyokuwa wamevaa.
Pia walipigwa picha kama wafungwa."Ingawa hakikuwa kifongo cha ukweli, lakini nilihisi kukosa uhuru" alisema Bob watson, mmoja wa watu waliolipa kulala jela.
Kila chumba kidogo ndani ya gereza hilo kina kitanda cha chuma na godoro jembamba, huku balbu yenye mwanga mdogo ikiwaka usiku kucha.
Hata hivyo kuna TV yenye channel moja ambayo haisikiki kutokana na kelele ndani ya gereza.
Konokono anaweza kupita kwenye ncha ya wembe bila kujikata.ungwa kwenu
0 comments:
Post a Comment