

KATIBU WA WAMILIKI WA DALADALA MKOA WA MOROGORO SAIMON RWAGAMUGIRA KUSHOTO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI JUU YA KUGHAILISHA MKUTANO HUO MKUU WA UCHAGUZI NA KULIA NI MWENYEKITI WA WAMILIKI WA DALADALA MKOANI HAPA, IDD MISSIGARO.
NA ESTER MWIMBULA MOROGORO.
UMOJA wa wamiliki wa daladala mkoa wa Morogoro (UWADAMO) wameshindwa kufanya mkutano wao mkuu wa uchaguzi wa viongozi na kutoa taarifa ya chama ya mapato na matumiza ya chama hicho toka mwaka 2008 hadi 2011 baada ya wanachama na wadau kushindwa kufika katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa chama hicho Iddi Misigaro alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kudai kuwa mkutano huo muhimu pia ulipangwa kwaajili ya kujadiri matatizo mbalimbali yanayoikabiri sekta hiyo ya usafirishaji mjini hapa.
Alisema kuwa kutokufanyika kwa mkutano huo kume sababishwa na kutokuhudhulia kwa wamiliki wa daladala bila ya kutoa udhuru wowowte licha ya kutoa taarifa kwao mapema kwa mmiliki.
Misigaro alisema kuwa uongozi uliokuwepo sasa madarakani umemaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ya chama hicho hivyo wanatakiwa kuuchia uongozi mwingine kwaajili ya kukiongoza chama hicho cha wamiliki wa daladala mkoani Morogoro baada ya kukaa madarakani kwa miaka mitatu toka mwaka 2008.
Alisema kuwa kutokufika kwa wamiliki hao kumewafanya uongozi huo uliomaliza muda wake kukaa madarakani hadi pale mkutano mkuu utakapoitishwa tena.
Naye katibu wa chama hicho Saimoni Rwamugira alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa chama hicho uongozi wao umefanikiwa kuleta maendeleo mbalimbali ndani ya chama hicho cha wamiliki wa daladala Mkoani Morogoro.
Aliyataja baadhi ya mafanikio walioyapata katika ungozi wao kuwa ni pamoja na kuondoa wapiga debe katika stendi ya mlali, kufungua akaunti ya chama kwenye benki ya NBC mkoani hapa, kujenga ofisi ya chama, pamoja na kutatua tatizo la ushuru wa getini .
Rwamugira alisema kuwa aliwaomba wamiliki wa daladala kuheshimu na kujitokeza katika vikao vya kujenga chama chao na pia wakumbuke kuwa wanahaki ya kujua mapato na matumizi ya chama hicho.
Pia alisema kuwa wamiliki wanapaswa kuwa karibu na viongozi wa chama hicho ili kujua maendeleo chama kuanzia kilipoanzishwa hadi sasa, kwani wamiliki waache tabia ya kwenda kwa viongozi hao pindi wanapotaka kutatuliwa matatizo yao tu.
0 comments:
Post a Comment