
Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amepinga hatua iliyochukuliwa na kundi la nchi na taasisi za kimataifa 40, kulitambua Baraza la Mpito la Waasi wa Libya kama chombo halali kinachowakilisha wananchi wa Libya.
Kundi hilo la mashauriano kuhusu Libya, lilikutana jana mjini Istanbul Uturuki. Katika mkutano huo, lilitangaza kutambuliwa kwa baraza la waasi kama mwakilishi wa watu wa Libya na " serikali yenye mamlaka". Marekani imeungana na mataifa mengine makuu kuwatambua waasi wa Libya kama chombo halali cha uongozi nchini Libya.
0 comments:
Post a Comment