BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANASOKA WA ZAMANI WAONYESHA KIWANGO MASHINDANO YA KAMANDA CHIALO CUP 2011 UWANJA WA SHUJAA MORO.

WANASOKA wa zamani waliowahi kutamba na klabu kubwa za soka mkoa wa morogoro wakiongoza na mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood wamekuwa kivutio kikubwa katika mashindano ya Kamanda Chialo Cup 2011 yanaendelea katika uwanja wa Shujaa mkoani hapa.

Mashindano hayo yaliyobeba ujumbe wa ulinzi shiriki polisi jamii kwa kushirikisha timu za soka 24 za Manispaa hiyo zikiwemo za vijana chini ya umri wa miaka 23 na timu zinazoshiriki ligi mbalimbali za TFF mkoani hapa wachezaji hao walionyesha uhodari wa kwa kutandaza soka la licha umri wao kuwatupa mkono dhidi ya vijana ambapo mashabiki wa soka walipata burudani hiyo wakati timu ya Moro Veterani ilipopambana na timu ya Kihonda Magolofani FC kwenye mashindano hayo.

Kivutio kikubwa kilikuwa kwa mbunge wa jimbo la Morogoro mjini ambaye muda mwingi alikuwa akihama nafasi yake ya kiungo mshambuliaji wa kati (8) na kutafuta mipira kutoka katika maeneo mbalimbali ya uwanja huo kwa lengo la kusaka mipira na kutoa pasi kwa washambuliaji wa timu yake jambo lililowafanya mashabiki kumshangilia muda wote pindi alipokuwa na mpira.

Katika dakika ya 15 kipindi cha kwanza mbunge huyo nurusa andike bao la kuongoza baada ya kupiga shuti la juu ambalo lilitoka sentemita chache langoni mwamba wa juu katika lango la wapinzani wao kufuatia kugongeana vena na beki wa timu hiyo ya Moro Veteran Juma Hamisi aliyepanda kusaidia mashambulizi.

kivutio kingine kilikuwa kwa mchezaji wa zamani wa klabu ya Tumbaku FC ya Morogoro Sadik Mbeta aliyekuwa akicheza katika nafasi ya kiungo wa kati (6) kwa kucheza vema nafasi hiyo akipokea mipira kutoka kwa walinzi na kutoa pasi kwa washambuliaji wa timu yake ambapo naye baadhi ya mashabiki waliohudhuria mchezo huo walisikika wakimsifia kwa kucheza nafasi hiyo kwa makini tofauti na kiungo wa timu pinzani.

"Mmoja wa mashaki hao alisikika akisema kuwa hawa wazee wanacheza vizuri kutokana na kutumia sana akili katika kutoa pasi na akili lakini tatizo lao ni kushindwa kumudu vema kasi ya vijana kutokana na mbio ambapo hali hiyo inatokana na umri lakini wakipata mpira unaona kabisa vijana wanahaha kutafuta mpira na wakati mungine kulazimika kucheza faulo" alisema Salim Hafifu.

Mchezaji mungine aliyekuwa akishangiliwa na mashabiki hao ni beki wa zamani wa klabu ya Reli Morogoro na Simba Sport Club, Adam Seleman kwa kumudu vema nafasi ya sentafu (5) kwa kuwadhibiti washambuliaji wa timu pinzani ya Kihonda Magolofani katika mchezo huo ambao walipoteza kwa kufungwa bao 3-0.

Naye Mratibu wa mashindano hayo Shomari Kunguge alitaja matokeo ya michezo mingine ilichezwa kuwa kwenye mashindano hayo kuwa ni timu ya Sabasaba Chipolopolo FC iliweza kupoteza mchezo wao dhidi ya timu ya Viwawa FC kwa kukubali kutandikwa bao 3-huku timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ya Mafisa Ramasi FC nayo ikiibuka na ushindi kwa kuilaza timu ya Assembly kwa bao 2-1.

Matokeo mengine ni timu ya Dandee ambayo nayo ilifanikiwa kuifunga timu ya Uhuru Rangers FC kwa bao 2-0, Maskani ikiishinda Mzinga kwa bao 2-0 na Kaizer Chief ikitandika timu ya Ulugwai kwa kuifunga bao 2-0.

Wakati timu ya Jamaica FC ilitoshana nguvu na Mikocheni kwa kutoka sare ya bao 1-1 huku Terminal ikiibuka na ushindi dhidi ya kazaroho FC na Atlas FC ikitoa sare ya bao 1-1 na Nanenane FC.

Mashindano hayo ambayo yamebeba ujumbe wa ulinzi shirikishi polisi jamii yanashirikisha timu 24 za Manispaa hiyo huku hatua ya makundi ikitarajia kumalizika septemba 1 mwaka huu kabla ya kuanza kwa hatua ya mtoano kwa timu 16 na kupata timu nane zitakazofuzu kucheza hatua ya robo fainali.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: