BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BENCHI LA UFUNDI KLABU YA YANGA KUNA TATIZO.

MWENYEKITI wa Yanga mkoa wa Morogoro Shomari Kunguge amesema ndani ya benchi la ufundi la klabu timu hiyo kuna matatizo ambayo uongozi wa juu unahitaji kutatua ili ushirikiano unaonyeshwa na wapenzi wa soka wa Yanga mkoa huo uwe na tija katika ligi kuu ya vodacom Tanzania bara mkoani hapa.

Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kumalizika kwa mchezo baina ya Yanga na Moro United uwanja wa Jamhuri Morogoro Kunguge alisema klabu ya yanga kwa sasa katika benchi la ufundi kuna matatizo ambayo uongozi wa juu wa klabu hiyo inailazimi kulifanya kazi suala hilo ili timu iwe na mshikamano kuanzia uongozi, benchi la ufundi na wachezaji.

Kunguge alisema matatizo hayo ameyaona katika michezo miwili ya ligi kuu ya vodacom mchezo wa Ruvu JKT ambao yanga ilitandikwa bao 1-0 na Yanga dhidi ya Moro United ambapo walitoa sare ya bao 1-1 huku meneja wa timu hiyo Silvatory Edward akiwa amekaa nje ya benchi la ufundi katika michezo hiyo yote.

Alisema hali ile sio mzuri kwa meneja wa timu kujiungua katika benchi la ufundi ambapo hali hiyo inaonyesha kutoelewana kwa benchi zima la ufundi na kudai pengeni hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa kutofanya vizuri kwa michezo hiyo miwili ambayo kwa Yanga imepoteza pointi tano muhimu katika ligi hiyo.

“uongozi wa yanga wakae na kuangalia hali hii kwani hivi sasa kuna tatizo katika benchi la ufundi haiwezekani meneja wa timu asikae katika benchi la ufundi wakati timu yake inacheza kuna nini hapa alihoji” Kunguge.

Hali ile kila wanachama, mashabiki na wampenzi wa klabu ya Yanga wameona vitendo vinavyofanyika katika benchi zima la ufundi la Yanga ambapo wakati mungine kumekuwa na upishi pindi mchezaji anapokata kubadilishwa kumekuwa na malumbano kati ya kocha mkuu Sam Timbe na Minziro ambalo hali hiyo ilijitokeza katika mchezo wa juzi dhidi ya Moro United juu ya mchezaji Godfrey Bon nani wa kutoka ili achukue nafasi yake kulikuwa na hali hiyo. Alisema Kunguge.

“uongozi wa yanga mkoa wa Morogoro tumekuwa tukijitahidi yanga ifanya vizuri lakini juhudi zetu zinakwamisha lakini kwa hii niliyoiona mimi lazima uongozi wa juu wa yanga ilifanyie kazi hii kwani benchi la ufundi hakuna maelewano kuanzia kocha mkuu, Msaidizi wake Silvesta Minziro na huyu Meneja Silvatory Edward hawa bwana hawaelewani tutapataje ushindi hapa kwa hali hii”. Alisema Kunguge.

Akizungumzia wachezaji Kunguge alisema wachezaji wa kigeni wamekuwa wakijituma kwa kiasi kikubwa lakini tatizo alioneka ni kwa wachezaji wazawa alidai wamekuwa wakicheza chini ya kiwango hivyo kama hali hiyo itaendelea basi Yanga itatema mapema ubingwa huo ambao wanautetea.

Katika klabu ya Yanga kwa sasa kuna daiwa kutokuwa na maelewano hasa katika benchi la ufundi na kudaiwa baadhi wachezaji wazawa kucheza chini ya kiwango ambapo katika mchezo wa ufunguzi kiungo mshambuliaji Nurdin Bakari na Rashid Gumbo hao ndio wanadaiwa kucheza chini ya kiwango huku katika mchezo dhidi ya Moro United Rashid Gumbo hakucheza mchezo huo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: