KOCHA mkuu wa klabu ya Moro United Hassani Banyai amesema sare walipata dhidi ya Yanga katika mchezo wa pili wa ligi kuu ya vodacom imeonyesha njia nzuri kwa timu yake katika harakati za kuwania ubingwa wa ligi hiyo iliyofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Akizungumza na mwandishi wa blogu hii katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro Banyai alisema amefurahishwa na kiwango kizuri walichoonyesha vijana dhidi ya Yanga katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri ambapo katika mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Banyai alisema kuwa mchezo ule ulikuwa nzuri na mgumu kwa upande wa timu yao lakini kutokana na wapinzani kuonyesha mchezo nzuri zaidi yao lakini baada ya Yanga kupata bao la kuongoza dakika ya 68 lililofungwa kiufundi na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Haruna Niyonzima kwa kichwa, vijana wake hawakukata tamaa, walitulia na kutandaza soka alilowafundisha na baadaye shangwe za mashabiki wa Yanga zilizimika dakika ya 87 kufuatia Jerome Lambele kufunga bao la kusawazisha kwa Moro United akiunganisha vema krosi ya Bakari Mpakala.
Alisema kuwa baada ya timu yake kupoteza mchezo wa ufunguzi wa lgi hiyo na Azam ambao Moro United ililala kwa bao 1-0 katika uwanja wa Chamazi Dar es Salaam na kupata sare na klabu ya Yanga ya bao 1-1 inaonyesha vijana wake wameanza kuelewana hivyo ana imani mchezo na Toto Afrika ya Mwanza utakuwa nzuri zaidi licha ya wao kushinda michezo miwili timu yake itaibuka na ushindi na kuondoka na pointi tatu muhimu mchezo utaofanyika uwanja wake wa nyumbani wa Chamazi Dar es Salaam.
“kama kocha mkuu mchezo walionyesha vijana wangu nimefurahishwa nao kwani kutoa sare na timu kubwa kama Yanga hiyo inaonyesha dalili njema kwatu kwani tulicheza vizuri ndio tukatoa sare na tukicheza hivi hivi kwa wachezaji kujitumka nini imani mchezo huo tutashinda dhidi ya Toto Afrika agosti 30 pale Chamazi” alisema Banyai.
Katika mchezo huo dhidi ya Moro United na Yanga walilazimika kusubiri hadi kipindi cha pili kupata bao la kuongoza kutokana na Moro United kuonyesha mchezo mzuri hasa katika safu ya kiungo na ulinzi kwa kuondoa hatari nyingi zilizoelekezwa katika lango lao huku Yanga ikionyesha mchezo mzuri kuanzia safu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji licha ya safu hiyo kupoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga mabao.
Katika mchezo huo Moro United itawategemea washambuliaji hatari wao kupachika mabao akiwemo Gaudenci Mwaikimba, mshambuliaji wa pembeni ya kulia Benidict Ngasa, Buji Seleman huku safu ya ulinzi ikiongozwa na nahodha wake Gidio Sepu, Tumba Swedy, Erick Mawala na katika lango likilindwa na mlinda mlango Lucheke Mussa.
Moro United mpaka sasa imepoteza mchezo mmoja na kutoa sare mchezo moja ikiwa na pointi moja huku Toto Afrika ya Mwanza ikiwa na pointi sita baada ya kushinda michezo miwili hiyo mchezo huo unatarajia kuwa mgumu kutokana na kila timu kujiweka katika nafasi nzuri katika ligi hiyo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment