UONGOZI wa timu ya soka ya Polisi Morogoro Sport Club iliyopo ligi dajara la kwanza imeshauriwa kuwashirikisha makocha wa mchezo huo kwa lengo la makocha hao kusaidiana na kocha aliyepo kusaidia kutoa mbinu mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya ligi hiyo kwa msimu wa mwaka 2011/2012.
Wakizungumza na gazeti hili wadau wa soka mjini hapa kwa nyakati tofauti katika mahojiano maalumu walisema uongozi wa jeshi la polisi mkoa Morogoro ipo haja kwa kuelekeza nguvu kwanza kwa kufanya usajili wa makini na kuwashirikisha kwa kuwaomba makocha waliopo ndani ya Manispaa ya Morogoro kutoa mbinu mbalimbali kwa wachezaji wakati wa mazoezi ambazo zitazosaidia kukabiliana na changamoto za mashindano ya ligi daraja la kwanza inayotarajia kuanza hivi karibuni.
Mmoja wa wadau hao Omari Mkwizu alisema kuwa timu ya polisi Morogoro ilipofikia kwa sasa ili kuweza kutafuta dawa ya kurejea ligi kuu ya Vodacom kwanza ni lazima uongozi mzima ukae na kutafakari namna ya kurejea ligi hiyo kwa kuanza kujenga mahusiano mazuri kwa kuwaomba makocha wasaidiane na kocha aliyepo kutoa mbinu kwa wachezaji wa timu hiyo ili timu hiyo iweze kufanya vizuri katika ligi daraja la kwanza.
“timu ya polisi ni mzuri ila ninavyoona mimi hawa viongozi wajipanga upya kwa ajili ya ligi daraja la kwanza lakini ili kurejea ligi kuu ya Vodacom itawalazimu kutumia mbinu mbalimbali ikiweo ya kusajili kwa umakini pia isisahau kuwashirikisha hawa makocha wa soka nao watoe mbinu kwa wachezaji wao kabla ya kuanza kwa ligi daraja la kwanza msimu huu” alisema Mkwizu.
Naye Rashidi Hassani alisema kuwa uongozi wa timu hiyo ya Polisi Morogoro unatakiwa kujifunza kutokana na timu hiyo kushindwa kurejea kwa ligi kuu ya Vodacom kwa misimu mitatu mfululizo ambapo hali hiyo ni funzo kwao.
Hassani alisema kuwa sio vibaya kwa uongozi wa Polisi Morogoro kuwashirikisha makocha hao ili nao wasaidie kutoa utalaamu wao kwa timu hiyo ambapo baada ya kuunda kamati iliyowashirikisha raia na askari waangalie na mbinu nyingine za mchezo huo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / WADAU WATOA MBINU YA KUREJEA LIGI YA VODACOM KWA VIONGOZI WA TIMU YA POLISI MOROMAANDALIZI YA LIGI DARAJA LA KWANZA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment