Mahakama moja nchini Taiwan imetoa amri kwa mwanamke mmoja kumlipa faini mchumba wake wa zamani kutokana na kumsababishia maumivu ya kiihisia.
Mahakama hiyo imetoa amri kwa mwanamke huyo kumlipa mchumba wake dola elfu nane baada ya kutotokea siku ya harusi yao.
Kwa mujibu wa BBC bi harusi huyo ambaye alikuwa na uja uzito wa miezi mitano wakati wa harusi alihitilafiana na mume wake mtarajiwa kutokana na mabishano ya nani wamualike na nani wasimualike katika harusi yao.
Mvutano huo ulikuwa mkubwa kiasi kwamba bi harusi akapanga kutokwenda katika harusi yake na kumuacha bwana harusi akiwa kasimama peke yake mbele ya wageni waalikwa.
Bwana harusi kuona hivyo alimshawishi mmoja wa wasichana wasimamizi wa harusi wafunge naye ndoa ili kuepuka aibu.
Hata hivyo wakati wakifunga ndoa hiyo ya kuepuka aibu, bwana harusi alibadili mawazo na kuamua kufunga ndoa ya kikweli kweli na msimamizi huyo wa harusi.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment