Waziri Mkuu wa Uturuki kutembelea Somalia
Waziri Mkuu wa Uturuki na familia yake wanatarajia kutembelea nchi ya Somalia hivi karibuni kwa lengo la kuifanya jamii ya kimataifa itoe mazingatio zaidi kwa nchi hiyo iliyokumbwa na baa la njaa.
Recep Tayyep Erdogan alisema kuwa atatembelea Somalia akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na familia yake na kujionea kwa karibu hali ya mambo ilivyo nchini humo.
Ameongeza kuwa ni jambo lisilokubalika kusimama kama watazamaji tu mbele ya maafa ya kibinadamu yanayotokea barani Afrika.
Ni nadra mno kwa viongozi wa nchi mbalimbali kutembelea Somalia kutokana na hali mbaya ya usalama katika nchi hiyo iliyoathiriwa vibaya na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Karibu nusu ya wakazi wa Somalia wanasumbuliwa na njaa na wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.
0 comments:
Post a Comment