BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UN: Waasi wa al-Shabaab wamedhoofika lakini huenda wakaungana upya

Umoja wa Mataifa umesema kundi la wanamgambo la al-Shabaab la Somalia lililouzigira mji wa Mogadishu mapema juma hili limedhoofika.

Augustine Mahiga, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika alisema kuwa kusimamishwa ufadhili na baadhi ya waungaji mkono wa al-Shabaab na mzozo kati ya makanda wakuu wa wanamgambo hao ndiyo mambo yaliyochangia katika kudhoofika kundi hilo la kigaidi linaloaminika kuwa na mfungamano na mtandao al-Qaida.

Hata hivyo Mjumbe huyo wa UN nchini Somalia ametahadharisha kuwa huenda wanamgambo hao wanatumia mbinu za kigaidi ambapo baadaye huenda wakauhujumu kwa kishindo mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.

Jumamosi iliyopita Rais Sheikh Shariff Sheikh Ahmed alitangaza ushindi mkubwa wa jeshi la nchi hiyo dhidi ya al-Shabaab baada ya wanagambo hao kuondoka mjini Mogadishu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: