YANGA, ARSENAL NA MAN U ZALAMBA DUMBE LEO.
Robin van Persie alifunga 'hat trick.
YANGA LEO IMETANDIKA SIMBA BAO 1-0 KATIKA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA BAO HILO LIKIWEKWA WAVUNI NA MSHAMBULIAJI HATARI RAIA WA KIGENI KUTOKA NCHINI ZAMBAI DAVIS MWAPE.
LIGI KUU YA UINGEREZA:
Mshambuliaji hatari wa Arsenal Robin van Persie amefunga mabao matatu wakati Arsenal ilipoichakaza Chelsea mabao 5-3 katika mchezo wa kusisimua uliochezwa katika uwanja wa Stanford Bridge.
Kiungo wa Chelsea Frank Lampard alikuwa wa kwanza kufungua mlango wa Arsenal kwa bao la kichwa lakini Van Persie akasawazisha muda mfupi.
John Terry akaipatia bao la pili Chelsea kwa mkwaju wa karibu kiasi cha yadi 16 kabla beki Andre Santos kusawazisha kipindi cha pili kwa mkwaju uliompita katikati ya miguu mlinda mlango wa Chelsea Petr Cech.
Theo Walcott aliiongezea uhai Arsenal kwa kufunga bao la tatu baada ya kupenya katika msitu wa mabeki wa Chelsea na Juan Mata baadae akaisawazishia Chelsea kwa kufunga bao la tatu kabla ya Van Persie kuongeza bao la nne katika lango lililokuwa wazi baada ya beki na nahodha wa Chelsea John Terry kuteleza.
Van Persie mabao yake mawili ya mwisho aliyafunga katika kipindi cha dakika tano.
Na baadae mshambuliaji huyo wa Arsenal akichezeshwa na Mikel Arteta kwa pasi murua dakika za nyongeza na akafumua mkwaju mkali ambapo mlinda mlango Petr Cech hakuweza kufanya lolote na kushuhudia nyavu zikicheza na kuiandikia bao la tano.
Ushindi huo umeiinua Arsenal hadi nafasi ya sita katika msimamo wa ligi.
MAN U.
Nayo Manchester United ilizinduka baada ya kipigo cha Jumapili iliyopita cha mabao 6-1 kutoka kwa Manchester City baada ya bao moja alilofunga Javier Hernandez kuwapa mshindi mgumu katika uwanja wa Everton.
Hernandez alitengewa mpira wa krosi kutoka kwa Patrice Evra katika dakika ya 19.
Bao hilo lilikuwa ni zawadi nzuri kutokana na kandanda nzuri waliyocheza United, lakini Everton walikuwa wakiisumbua sana Manchester United katika dakika zote zilizosalia.
Leighton Baines wa Everton alikosa bao baada ya mkwaju wake wa adhabu ndogo kugonga mwamba na mkwaju wa Louis Saha nao hakukuweza kulenga lango.
Matokeo hayo yameiimarisha Manchester United katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 23.
0 comments:
Post a Comment