BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHIPUKIZI AIBUKA MSHINDI WA KWANZA MASHINDANO YA PIKIPIKI YA KUVUKA VIKWAZO MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA KRISMAS MORO

ABDUL SALU (20)AKITEMBELEA TAILI MOJA LA NYUMA HUKU LA MBELE LIKIWA LIMENYANYUKA WAKATI WA MASHINDANO YA PIKIPIKI YA KUVUKA VIKWAZO WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA KRISMAS KATIKA UWANJA WA SABASABA MJINI MOROGORO.


KIJANA ALLY KIBOGOYO (17) AKIONGOZA MBIO ZA MASHINDANO YA PIKIPIKI WAKATI WA KUVUKA VIKWAZO KATIKA MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA KRISMAS YALIYOFANYIKA DESEMBA 25 MWAKA HUU UWANJA WA SABASABA MKOANI MOROGORO.

MWENDESHA pikipiki chipukizi, Ally Kibogoyo (17) ameibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya mbio za pikipiki za kuvuka vikwazo kutafuta mkimbiaji wa mchezo huo uliofanyika wakati wa kilele cha sikukuu ya krismas uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro.

Katika mashindano hayo ambayo yaliandaliwa na kampuni ya michezo ya Tembo Sports Promotion yalikuwa na lengo la kuibua vipaji vipya vya mchezo wa pikipiki na kuendeleza michezo ndani ya mkoa wa Morogoro.

Akizungumza na BLOGU hili katika uwanja wa Sabasaba mjini hapa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hamis Hamidu alisema kuwa kwa sasa wameweka mikakati kabambe ya kuibua na kuendeleza michezo ya aina tatu ikiwemo ngumi za kulipwa, mbio za pikipiki na michezo ya mbio za baiskeli huku lengo kuu la kampuni hiyo likiwa kutafuta vijana wenye vipaji vya michezo hiyo na kujipatia faida kutokana na michezo hiyo ikiwa njia mojawapo ya wao kujipatia kipato halali.

Hamidu alisema kwa sasa mwamko wa vijana kujitokeza katika kuingia katika michezo hiyo umekuwa mkubwa kwani tayari kundi la vijana hao wameanza kutambua faida zitokanazo na michezo na kuwa lichobaki kwao ni kuandaa michezo ambayo imekuwa ikiongeza mashabiki siku hadi siku.

Naye Mkufunzi wa mchezo wa mbio za pikipiki katika Manispaa ya Morogoro, Hussein Makusi alisema kuwa katika mchezo huo mwendesha pikipiki chipukizi Ally Kibogoyo ndiye aliyeibuka mshinda wa kwanza dhidi ya wapinzani wake sita baada ya kufanikiwa kuongoza mara tatu katika mbio hizo.

Makusi alisema kuwa chipukizi huyo aliweza kuwashinda wenzake katika mbio za kuvuka vikwazo akiongoza kwa kushika nafasi ya kwanza mara tatu huku aliyeshika nafasi ya pili Hamis Kiangala (20) akishinda mara mbili.

Alitaja aliyeshika nafasi ya tatu kuwa ni Abdul Salu (20) wakati nafasi ya nne ilichukuliwa na Kazy Mohamedi (27) ambapo mashindano yalishirikisha washiriki kutoka wilaya ya Kilomero na Manispaa hiyo ya Morogoro.

Washiriki wengine walioshiriki shindano hilo ni mkongwe Alpha Mtakwa (34), Hashim Masikini (26) na Perezi Baraka (20) ambao hawakuweza kufanikiwa kushinda hata mzunguko mmoja kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya pikipiki zao kuleta hitilafu katika mfumo wa umeme.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: