Fursa ya mwisho ya kumkamata Bush akiwa Afrika
BAADA ya Tanzania na Zambia kukaidi matakwa ya Amnesty International ya kumkamata mtawala wa zamani wa Marekani George W Bush, fursa ya mwisho ya kumtia nguvuni mtenda jinai huyo itajitokeza wakati akiwa nchini Ethiopia.
Kabla ya Bush kuanza safari yake ya siku tano ya kuzitimbelea nchi tatu za Afrika iliyoanza Desemba mosi, Amnesty International ilitoa wito kwa Tanzania, Zambia na Ethiopia kumtia mbaroni rais huyo wa zamani wa Marekani kutokana na jinai alizotenda akiwa madarakani. Bush atakuwa Ethiopia Desemba nne na tano.
Amnesty International imesema sheria za kimataifa zinasema watenda jinai za kivita hawapaswi kuwa huru na kwa hivyo ni wajibu wa nchi atakazotembelea kumtia nguvuni Bush.
Mtawala huyo wa zamani wa Marekani anadai yuko Afrika kuwasaidia wagonjwa wa Ukimwi, Malaria na Saratani katika hali ambayo alishusika katika mauaji ya mamia ya maelfu ya raia wakiwemo wanawake na watoto wasio na hatia Iraq, Afghanistan na maeneo mengine ya dunia.
Mapema mwaka huu Bush alifutilia mbali safari yake huko Uswisi baada ya hofu kuwa angetiwa mbaroni kutokana na jinai alizotenda akiwa rais tokea mwaka 2001 hadi 2009.
Mwezi uliopita Mahakama ya Kimataifa ya Jinai za Kivita ya Kuala Lumpur ilitoa hukumu kuwa Bush na Waziri Mkuu wa Zamani wa Uingereza Tony Blair wana hatia ya kuhusika na jinai dhidi ya binaadamu katika vita vya Iraq.
0 comments:
Post a Comment