Ndege za kivita za Kenya zashambulia tena Somalia
Ndege za kivita za Kenya zimetekeleza mashambulizi huko Somalia ambapo zimedaiwa kulenga kambi ya wakimbizi kusini mwa Somalia na kusababisha watu kadhaa kuuawa na kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa mwandishi wa Radio Tehran nchini Somalia, mashambulizi hayo ya angani yamelenga kambi ya wakimbizi katika eneo la Gedo kijijini Ceel Ade siku ya Ijumaa alasiri.
Mkuu wa eneo la Gedo Mohamad Abdi Kalil amethibitisha kutokea hujuma hiyo.
Kenya ina karibu wanajeshi elfu nne katika ardhi ya Somalia waliotumwa nchini humo katikati ya mwezi Oktoba mwaka huu ili kupambana na waasi ash Shabab wanaotuhumiwa na serikali ya Nairobi kwamba, wanahatarisha usalama wa Kenya.
Serikali ya mpito ya Somalia imetangaza kuunga mkono kampeni ya Kenya dhidi ya waasi ash-Shabab.
0 comments:
Post a Comment