BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MASHINDANO YA SHIMIVUTA 2011.

Mshambuliaji wa timu ya soka ya chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) Frank Mkomwa kushoto akiwatoka wachezaji wa taasisi ya elimu ya watu wazima Dar es Salaam (IAE) Laurent Kansola (chini) na Eliud Waliha wakati wa mashindano ya shirikisho la michezo ya vyuo vya elimu ya juu Mchanganyiko Tanzania katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo katika mchezo huo IFM ilishinda kwa bao 3-0.




Juma Mdee wa timu ya soka ya taasisi ya elimu ya watu wazima Dar es Salaam (IAE) kushoto akiwania mpira dhidi ya Edwin Kavishe wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) wakati wa mashindano hayo.

MASHINDANO ya shirikisho la michezo kwa vyuo vya elimu ya juu mchanganyiko Tanzania
(SHIMIVUTA) yameanza kutimua vumbi desemba 9 katika viwanja vitatu tofauti ikishirikisha michezo mitano mkoani Morogoro.

Akizungumza na gazeti hili katibu mkuu wa SHIMIVUTA uwanja wa Jamhuri mkoani hapa, Augustino Matem alisema mashindano ya mwaka huu ya shirikisho hilo limeshirikisha jumla ya vyuo 14 vya elimu ya juu mchanganyiko Tanzania ambapo mashindano hayo yameanza kutimua vumbi desemba 9 na kumalizika desemba 18 kwa michezo yote ambayo yanafanyika viwanja vitatu tofauti mkoani hapa.

Matem alisema kuwa michezo ambayo wanamichezo wanashiriki ni pamoja na soka iliyogawanywa makundi mawili, netiboli, kikapu, wavu na riadha ambayo inafanyika kwenye viwanja vya chuo cha ujenzi Morogoro, Bwalo la umwema na Jamhuri.

Alisema kuwa kwa upande wa uwanja wa jamhuri na chuo cha ujenzi michezo ambayo imekuwa kichezwa ni pamoja na soka, netiboli na riadha wakati katika uwanja wa Bwalo la Umwema ni michezo ya wavu na kikapu.

Alitaja vyuo ambavyo vimeleta timu kuwa ni chuo cha elimu ya biashara (CBE), chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru Arusha (CDTI) chuo cha serikali za mitaa (LGTI) Chuo cha ufundi Arusha (ATC), Chuo cha ustawi wa jamii Dar es Salaam (ISW) na chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

Alitaja vyuo vingine kuwa ni chuo cha usimamizi wa fedha (IFM), taasisi ya teknolojia Dar es Salaam (DIT), chuo cha uhasibu Tanzania (TIA), chuo cha uhasibu Arusha (IAA) chuo cha mwalimu nyerere kivukoni (MNMA), Taasisi ya elimu ya watu wazima Dar es Salaam (IAE), chuo cha mipango na maendeleo vijijini (IRDP) na chuo cha sayansi na teknolojia Mbeya (MIST).
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: