BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ZAIDI YA FAMILIA 75 MAFISA HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MILIPUKO ENDAPO JUHUDI ZA KUDHIBITI MAFURIKO HAZITACHUKULIWA MORO.


MWENYEKITI WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF)KATA YA MAFISA MANISPAA YA MOROGORO AMIR KINYANSI AKIRUKA MOJA YA SEHEMU YA KINGO ZA MTO MOROGORO IMEBOMOLEWA NA KUSABABISHA MAJI KUELEKEA KATIKA MAKAZI YA WATU WAKATI WA ZIARA YA KIONGOZI HUYO NA WAKAZI WA MTAA WA SINA KATA HIYO AMBAYO WAMEKUWA WAKIKUMBWA NA MAFURIKO YANAYOTOKANA NA TATIZO HILO MKOANI HAPA.

ZAIDI ya familia 75 za wakazi wa mtaa wa Sina kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro ziko katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya milipuko endapo juhudi za haraka hazitochukuliwa kudhibiti mafuliko yaliyozikumba familia hizo kutokana na kingo za mto mto ya Morogoro kubomoka.

Akizungumza na wakazi waliokumbwa na mafuriko hayo mjini hapa Mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) kata ya Mafisa, Amiri Kinyansi alisema serikali inapaswa kuangalia uwezekano wa kuziba kingo za mto huo zinazochangia mafuriko hayo ambazo zinadaiwa zimekuwa zikivunjwa na watengeneza matofali na wakulima wa mabongeni.

Kauli hiyo imetolwa wakati wa ziara ya kiongozi huyo ya kuwatembelea walioathirika na mafuriko hayo na kubaini kuwa kingo za mto huo zilizobomolewa haziwezi kujengwa na wananchi pekee na kwamba jitihada za serikali zinahitajika.

Kinyansi alisema kuwa kwa tathimini iliyofanyika na wakazi hao wamebaini uwezekano wa wananchi hao kupata magonjwa ya milipuko kutokana na maji hayo kusomba uchafu mwingi ambao umekuwa ukituama katika makazi yao ikiwemo na kinyesi cha binadamu.

Naye mmoja wa wakazi wa mtaa huo, Shariffa Ramadhan (54) alisema kuwa tatizo hilo limekuwa la muda mrefu licha ya wakazi hao kutoa taarifa za kuomba msaada serikalini ili kuzibwa kwa sehemu zilizobomolewa lakini mpaka sasa viongozi wameshindwa kutatua kero hiyo.

Ramadhan alisema kuwa sio ajabu kukuta kinyesi cha binadamu katika makazi yako hasa kipindi cha mvua ambacho kimesombwa na mafuriko na kudai hali hiyo inawafanya wakazi wa mtaa huo kuwa hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko.

“sehemu zilizobomolewa na wakulima wa zao la mpunga na hawa vijana wanaofyatua matofali zinaweza kudhibitiwa kabisa ila tatizo viongozi wetu wa serikali ya mtaa hadi kata hawapendi kusikiliza kero za wananchi kwani tumetoa taarifa juu ya adha tunayopata ambayo imetokana na kubomolewa kwa kingo za mto Morogoro lakin wameshindwa kufika eneo la tukio, sasa sijui wanasubiri maafa yatokee ndio waje”, Ramadhan.

Mmoja wa viongozi wa serikali ya mtaa wa Sina, John Swea alipoulizwa na mwandishi wa habali hii kwa njia ya simu juu ya kero hiyo ya wakazi wa mtaa huo kukumbwa na mafuriko na kutoa taarifa katika ofisi yake mwenyekiti huyo alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa njia ya simu hivyo mwandishi atafute nafasi ya kwenda ofisini kwake ili akaulize swali hilo.

Mwandishi wa habari hii ameshuhudia uharibifu mkubwa wa mazingira uliofanywa kutokana na uchimbaji wa udongo unaotumika kwa ufyatuaji matofali na kilimo kandokando ya kingo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: