WANAJESHI WA DJIBOUTI WAWASILI SOMALIA KUUNGANA NA VIKOSI VYA UMOJA WA AFRIKA ILI KUKING'OA KIKUNDI CHA WANAMGAMBO WA AL-SHABAAB.
Kikosi cha kwanza cha wanajeshi 100 kutoka Djibouti kimewasili Mogadishu jana kuungana na vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) vinavyopigana na makundi ya al-Shabaab yenye mahusiano na al-Qaeda.
Wanajeshi wengine 800 watawasili wiki ijayo au baadae. Wanajeshi hao wa Djibouti wanaozungumza Kisomali, watashirikiana na wanajeshi 9,800 kutoka Burundi na Uganda waliopo Somalia tangu mwaka 2007 kuilinda serikali ya Somalia katika mji mkuu Mogadishu.
Brigedia-Jenerali Audace Nduwumunsi wa vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia amesema, kuwasili kwa kikosi hicho cha Djibouti ni hatua kubwa kwa AMISOM na jitahada za kuleta utulivu nchini Somalia.
0 comments:
Post a Comment