WATU 46 NIGERIA WAUWAWA KWA SHAMBULIO
Inaarifiwa kuwa mripuko kwenye kanisa la Kikatoliki katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, umesababisha hasara.
Muuguzi mkuu katika hospitali ya hapo alisema hali ni mbaya sana.
Majeruhi wanahamishiwa mahospitali makubwa; lakini inasemekana magari ya kusaidia majeruhi ni machache.
Ibada nyingi makanisani hazikufanywa katika eneo hilo ambalo wakaazi wake wengi ni Waislamu kwa sababu ya mapambano baina ya wanajeshi na watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kikundi cha kiislamu cha Boko Haram.
Kasisi Joseph Hayet ni mshauri wa maswala ya Wakristo kwa serikali katika jimbo la Kaduna.
Aliiambia BBC kuwa usalama umezidishwa katika jimbo hilo kwa sababu ya Krismasi:
"Nimezungumza na makanisa leo asubuhi.
Walichoniambia ni kuwa watafanya ibada fupi sana, hawatazifanya ndefu; na watachukua hatua za usalama kuhakikisha kuwa hakuna anayeingia.
Taarifa moja tuliyopata ni kwamba wale wanaokusudia kuleta mtafaruku huu wanakuja na piki-piki na kurusha mabomu makanisani.
Kwa hivo makanisa yanachukua hatua kuhakikisha kuwa piki-piki hazikaribii, na hivo hawatoweza kurusha mabomu makanisani"
Taarifa nyengine kutoka Nigeria zinaeleza kuwa miripuko mengine imetokea katika miji mengine, katika eneo la kaskazini.
Ripoti moja inasema kikundi cha Kiislamu cha Boko Haram kinasema kuwa kilifanya shambulio la awali katika mji mkuu, Abuja.
0 comments:
Post a Comment