MTIBWA SUGAR YATANDIKWA NA POLISI MORO MAANDALIZI YA LIGI KUU JAMHURI MORO.
MSHAMBULIA NICOLAUS KABIPE AKICHUANA NA JUMA ABDU KATIKA MCHEZO WA KIRAFKI WA KUJAIANDAA NA LIGI KUU YA VODACOM KWA MTIBWA SUGAR WAKATI POLISI MORO WAKIJIANDAA NA LIGI DARAJA LA KWANZA.
MSHAMBULIA WA POLISI MORO NICOLAUS KABIPE AKICHUNA NA MLINZI WA MTIBWA SUGAR SALUM SUED KUSI WAKATI WA MCHEZO HUO.
MSHAMBULIAJI WA POLISI MOROGORO SPORTS CLUB, ABDALLAH JUMA KUSHOTO AKICHUANA NA MCHEZAJI WA MTIBWA SUGAR YA MANUNDU TURIANI, THOMAS MOURICE WAKATI WA MCHEZO WAO WA KIRAFIKI WA KUJIANDAA NA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA AWAMU YA PILI KWA MTIBWA WAKATI POLISI WAKIJIANDAA NA LIGI DARAJA LA KWANZA HATUA YA PILI PIA AMBAPO KATIKA MCHEZO HUO MTIBWA ILIKUBALI KIPIGO CHA BAO 2-1 UWANJA WA JAMHURI MOROGORO.
KLABU ya soka ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani imekubali kipigo kutoka kwa Polisi Morogoro SC inayojindaa na ligi daraja la kwanza katika mchezo mkali wa kirafiki na kusisimua kwa bao 2-1 uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Katika mchezo huo ambao Mtibwa Sugar ilitawala sehemu kubwa katika vipindi vyote vya mchezo huo kilishindwa kutumia vema nafasi walizopata kwa kufunga langoni mwa wapinzani wao na kujikuta wakitandikwa bao 2-1 na Polisi Moro SC katika dakika ya 66 n 85 huku bao la Mtibwa Sugar likipatikana katika dakika ya 89.
Kikosi cha Kocha Mkuu wa klabu ya Polisi Morogoro, John Simkoko ndicho kilichoonekana kuwa na malengo zaidi hasa baada ya washambuliaji wake kutumia vema nafasi walizopata kufunga mabao hayo huku Mtibwa Sugar wakipoteza nafasi nyingi za kufunga.
Bao la kwanza la Polisi Morogoro lilifungwa na mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Abdallah Juma dakika ya 66 baada ya kazi mzuri ya mshambuliaji, Nicolaus Kabipe kudokoa mpira kwa mlinzi Salum Sued wa Mtibwa Suga na kumkuta mfungaji wakati bao la pili lilipachikwa wavuni na Nicolaus Kabipe kufuatia kuuwahi mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Mtibwa Sugar, Khameiny Abdubakari dakika ya 85 na kuandika bao la pili.
Baada ya kutandikwa mabao hayo mawili Mtibwa Sugar walipata bao lao la kufutia machozi kwa mpira mferu wa juu uliopigwa na mshambuliaji, Kessy Kidangile dakika ya 89 ambao kabla ya kuingia kwa bao hilo mchezaji, Saidi Banuzi aliruka juu na mlinda mlango wa Polisi Morogoro Kondo Salum kuwania mpira huo kabla ya kujaa wavuni na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Mtibwa Sugar kupoteza kwa bao 2-1.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa maandalizi ya timu hizo huku Mtibwa Sugar ikijiandaa na ligi kuu ya Vodacom mzunguko wa pili wakati Polisi Morogoro nayo ikijiandaa na ligi daraja la kwanza hatua ya pili ambapo ligi hizo zinatarajia kuanza hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment