BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE KALOGERIS AKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 85 YENYEN THAMANI YA MATENGEZO SH 4.2MIL KIJIJI CHA KIGANILA MORO VIJIJINI.


Kalogeris akihutumia wananchi katika mkutano huo katika kijiji cha Kiganila wilaya ya Morogoro Vijijini.


Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini kupitia CCM, Inocent Kalogeris (mwenye sharti ya kijani) akimkabidhi msaada wa moja ya madawati 85 Mwenyekiti wa kijiji cha Kiganila, Athman Nyumbo.

MBUNGE wa jimbo la Morogoro Kusini kupitia CCM, Inocent Kalogeris amekabidhi msaada wa madawati 85 yenye thamani za matengenezo Sh4.2Mil kwa uongozi wa kijiji cha Kiganila baada ya wananchi wa kijiji hicho kukamata mazao ya misitu katika msitu wa hifadhi wa Mkulazi kilichopo kata ya Selembala tarafa ya Mvuha mwaka 2011 Morogoro Vijijini.

Upatikanaji wa madawati hayo yametokana na juhudi za wananchi wa kijiji hicho kulinda na kuhidhali maliasili zinazowazunguka sanjali na umoja wao wa ulinzi shirikishi ambao ulisaidia kubaini mapema wizi na utoroshaji wa mazao ya misitu zikiwemo mbao na magogo ambayo yalivunwa kwa kukiuka sheria za uvunaji wa mazao hayo ambapo mbunge huyu alikubaliana na uongozi wa serikali ya kijiji kutengeneza madawati kwa ajili matumizi ya shule ya kijiji hicho.

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa hadhala uliofanyika kijijini hapo, Kalogeris alisema kuwa anawapongeza wananchi wa kijiji hicho cha Kiganila kwa mwamko wao waliokuwa nao wa kubaini upotevu wa mali za asili hasa baada ya kukamata mbao na magogo ambayo yalivunwa kwa njia ya wizi na juhudi za kutoroshaji mazo hayo kushindikana hivyo faida ya kukamata mazao hayo umesaidia upatikanaji wa madawati 85 na wanafunzi watapata nafasi ya kutumia wakati wa masomo yao.

“Tuna kero nyingi sana katika kijiji hiki lakini baadhi ya kero tayari tumeanza kuzitatua ikiwemo la upatikanaji wa madawati 85 hili tumemaliza ambapo kwa upande wa zahanati ya serikali ya kijiji cha Kiganila nayo ipo katika hatua za mwisho za ujenzi wake hivyo inatulazimu kujipanga kwa ajili ya kuangalia namna ya kukarabati barabara zetu ili ziweze kupitika wakati wote bila ya kuwa na vikwazo hivyo ninachoomba kwenu muendelee kutoa ushirikiano ili tujenge maendeleo katika jimbo letu” alisema Kalogeris.

Wakati huo huo mbunge huyo ametoa wito kwa wakazi wa kijiji hicho kujitokeza kwa wingi katika ziara ya Rais Jakaya Kikwete ambapo anatarajia kuja katika tarafa ya Matombo na Mvuha kwa ajili ya uzinduzi wa miradi minne ikiwemo kuzindua rasmi madaraja mawili ya Mtombozi na Magogoni kabla ya kuweka jiwe la msingi soko la kisasa la mji mdogo wa Matombo na ukakuguzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 5.8.

Rais Kikwete (januari 17) kesho atazinduzi miradi minne katika wilaya ya Morogoro Vijijini katika madaraja mawili ya Mtombozi na Magogoni sambamba na kuweka jiwe la msingi soko la Matombo na kuangalia barabaraba inayotengezwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 5.8 hivyo wananchi wajitokeze katika maeneo hayo kushuhudia uzinduzi huo na uwekaji wa jiwe la msingi. alisema Kalogeris.

Akifafanua zaidi juu ya ziara hiyo kwa wananchi Kalogeris alisema kuwa wananchi wajitokeze kwa wingi kuanzia katika eneo ya njiapanda ya barabara ya msalabani ambapo ndipo ataanza kwa kukagua ujenzi wa barabara, kuweka jiwe la msingi soko jipya la Matombo kabla ya kuelekea njiapanda ya barabara ya Mtombozi ambapo ataenda kuzindua daraja la Mtombozi kisha daraja la Mgogoni.

Katika mkutano huo mbunge wa jimbo hilo la Morogoro Kusini, Inocent Kalogeris ulisitishwa kutokana na ujio wa rais Kikwete kwa ajili ya uzinduzi wa miradi minne ya kuzindua madaraja mawili ya Mtombozi yanyounganisha vijiji vya Nemele huku daraja la Mgogoni likiunganisha Ngerengere na kuweka jiwe la msingi soko la mji mdogo wa Matombo na kukagua barabara yenye urefu wa kilometa 5.8 inayojengwa kwa kiwango cha lami inayoanzia njiapanda ya Msalabani hadi njiapanda ya Mtombozi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: