BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NAFAFANUA JAMBO LA COMPASSION INTERNATIONAL TANZANIA.


MKURUGENZI WA NCHI SHIRIKA LA COMPASSION INTERNATIONAL TANZANIA MCHUNGAJI, JOSEPH MITINJE AKIFAFANUA JAMBO WAKTIKA UZINDUZI HUO.

MKUU wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera amezinduamradi wa matanki 11 ya maji safi na salama wenye thamani ya sh 59.2Mil kwaajili ya vituo 11 vya kutoa huduma ya Mtoto katika shirika la CompassionInternational Tanzania wanaishi katika mazingira magumu mkoani hapa.

Katika shirika hilo la Compassion InternationalTanzania mradi huo umeinufaisha watoto 3630 kwa mkoa wa Morogoro kupata hudumaya maji ukilenga kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji ya kutoshakwenye vituo hivyo ambapo matanki hayo yana ujazo wa kuhifadhi maji lita10,000 kila moja.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo katikakanisa la TAG Gosheni Kilakala Manispaa ya Morogoro, Bendela alipongeza shirikahilo kwa juhudi hizo kwani upatikanaji wa maji ndani ya Manispaa ya Morogoro nisawa na 22.8% kwa wakazi wake hivyo mradi huo utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizola upatikanaji wa maji kwenye vituo hivyo.

Bendela alieleza kuwa juhudi zilizochukuliwa najumuiya ya makanisa 11 ya kiinjilri kushirikiana na shirika la compassionInternational Tanzania kuendeleza kutoa huduma ya kijamii katika kuwaendelezawatoto kielimu kutoka elimu ya msingi mpaka chuo kikuu kwa familia maskini nijambo la kuunga mkono na mashirika mengine hapa nchini.

“kwa kweli juhudi mnazofanya serikali inawapongezasana katika kutoa huduma za kijamii ili kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumlahasa watoto wasiojiweza na changamoto ambazo mnazokabiliana nazo tutajitahidibega kwa bega ili tuweze kuzitatua kadiri ya uwezo wetu”. alisema Bendela.

Naye Mkurugenzi wa Nchi shirika la compassion International Tanzania Mchungaji,Joseph Mitinje alisema kuwa shirika la Compassion International ni shirika lakikristo la kimataifa la kuhudumia watoto walio katika mazingira magumu kwanjia ya ufadhili kwa lengo la kuwawezesha watoto walio katika mazingira magumukutokana na umaskini kupata huduma kama watoto wengine wenye wazazi ambaowanakipata.

Vituo vilivyofaidika na mradi huo wa matanki ya majihayo ni pamoja na FPCT Kihonda,TAG Ebenezer, TAG Bethel Mwembesongo, TAGGosheni Kilakala, TAG Mazimbu, ATCT Mtoni Street, FPCT Kihonda Ukumbi wa MfalmeSuleiman, KMT Mennonite Kigurunyembe, EAGT Chamwino, Moravian Kiwanja chaNdege, Railways Station, Anglikana Holytrinity Manzese.

Mitinje alisema kuwa katika shirika hilo limejikita zaidi katika mpangowa Kunusuru Maisha ya Mama na Mtoto kwa kutambua kwamba umaskini ni janga na linawezakuwafanya watoto wasifikie umri wa miaka 5 kwa magonjwa ambayo yangewezakutibika na kuzuilika ambapo Compassion International Tanzania lilianza mpangompya wa kunusuru maisha ya mama na mtoto tangu mwaka 1999 hapa nchini.

“Mpango huu hulenga akina mama maskini ambaoni wajawazito na wale wenye watoto chini ya umri wa miaka 3 ambapo tumekuwatukiwalea watoto wao salama na hatimaye waweze kusajiliwa katika mpango waufadhili wa mtoto mpaka sasa tuna akina mama 1,003 na watoto wapatao 1,011wanaohudumiwa katika mpango huu” alisema Mitinje.

Shirika hilo hapa nchini lilianzishwa April 1999 katika mkoa wa Arusha na kuanzakuhudumia watoto 3,000 ambapo limejipanua kufika mikoa 12 ya Tanzania hukuikihudumiaidadi ya watoto 65,000 ambao wapo kwenye vituo 250 katika mikoa ya Arusha,Manyara, Kilimanjaro, Singida, Pwani, Tabora, Iringa, Shinyanga, Morogoro,Dodoma, Mwanza, na Mara.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: