
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, ADAMU KIGOMA MALIMA PICHA YA MAKTABA.
Na Venance George, Morogoro
NAIBU Waziri wa nishati na madini Adam Kigoma Malima ameibiwa vitu mbalimbali alivyokuwa navyo katika hoteli ya nyota nne ya Nashera ya mjini Morogoro alikokuwa amefikia mara baada ya ziara yake ya siku mbili mkoani Morogoro.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro, lilitokea majira ya saa 10.45 alfajiri ya kuamkia jana ambapo mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichokuwa naibu waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu vyenyathamani ya zaidi ya Sh23.3 milioni.
Vitu hivyo vinajumuisha laptop tatu aina ya Dell zenyethamani ya Sh5.6 milioni, digital recorder mbili na headphone zake zote zikiwa Na thamani ya Sh1 milioni, simu tatu Nokia C6 ya Sh500, 000, Nokia E200 ya Sh250, 000 na Blackberry ya Sh5.5 milioni.
Vingine ni pete mbili za silva zenye thamani ya Sh2.5 milioni, fedha taslimu dola za kimarekani 4,000 (Sh6.5milioni), fedha za kitanzania Sh1.5 milioni, kibagalashia chenye thamani ya Sh50,000 kadi mbili za benki, mabegi matatu, moja la nguo na mengine ya kompyuta na nyaraka mbalimbali za serikali.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Hamisi Seleman aliwaambia waandishi wa habari kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.
Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Morogoro alisema kuwa hata hivyo mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuweza kuiba siraha aina ya Bastola na SMG alizokuwa nazo naibu waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.
Alisema kuwa mpaka sasa polisi inawashikilia walinzi watatu kwa mahojiano zaidi kutokana na tukio hilo kwa madai kuwa wao ndiyo wenye dhamana ya ulinzi wa eneo hilo.
Hata hivyo, Selemeni alisisitiza kuwa mtaalam wa kamera za ulinzi za hoteli hiyo pia anaendelea kufanya utafiti ili kubaini kama kunapicha zilizonaswa na kamera hizo wakati wa tukio hilo.
“Ukitazama vizuri katika picha cha kamera hizo unakivuli cha gari inaonekana upande wa barabarani, lakini bado haioneshi wazi ni aina gani ya gari, hivyo tunaendelea kuchunguza,”alisema.
Alfajiri baada ya kuzagaa kwa taarifa hiyo viongozi wa serikali mkoani hapa akiwemo mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na katibu tawala wa mkoa huo, Mgeni Baruani na maafisa usalama kufika katika hoteli hiyo.
Waandishi wa habari walifika katika hoteli hiyo majira ya saa 3.22 asubuhi wakitaka kujua kilichojiri ambapo uongozi wa hoteli hiyo uliwazuia waandishi hao kumwona naibu waziri wakidai kuwa alikuwa na mazungumzo na viongozi wengine na waandishi hawakuruhusiwa kumwona kwa wakati huo.
Waandishi hao ili wachukua muda wa nusu saa wakiwa wamekaa eneo la mapokezi ya hoteli hiyo wakingoja mpaka hapo walipolazimika kumpigia simu mkuu wa mkoa wa Morogoro aliyekuwa na naibu waziri huyo na kuwaruhusu kwenda kumuona.
Hata hivyo, wakiwa wanaelekea huko waandishi hao walikutana na kikwazo kingine cha walinzi wa hoteli hiyo wakiongozwa na msimamizi wa nyumba, Advent Kweka, kuwazuia waandishi hao wasiende kumwona naibu waziri huyo wakiwataka waandishi hao kurejea mapokezi na naibu waziri atakutanao hao hapo.
Muda mfupi baadaye mkuu wa mkoa wa Morogoro akiwa ameongozana na katibu tawala wa mkoa na maafisa usalama wa taifa walijitokeza mbele za waandishi wa habari na kuwaambia waandishi kuwa isingekuwa vema kwenda kumwona naibu waziri chumbani kwake kwa vile huko ni mahali pa faragha zaidi.
“Sisi tumepata taarifa na tulikuja kumpa pole. Siwezi kuwa msemaji wa jambo hili kwa vile mwenye kupaswa kulitolea ufafanuazi ni naibu waziri mwenyewe au hata meneja wa hoteli ambaye ndiye mkuhusika mkuu kwa vile tukio hili limetokea katika hoteli yake, “ alisema mkuu huyo wa mkoa.
Kwa upande wake meneja wa hoteli ya Nashera, Eustini Mtua, alikiri kutokea kwa tukio hilo lakini akadai kuwa hakuwa tayari kulitolea ufafanuzi zaidi kwa vile polisi walimzuia kutotoa taarifa yoyote mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika.
“Kwa sasa sitapenda kusema kitu chochote kwa vile hivi tunavyozungumza sasa polisi wanaendelea na uchunguzi wao na wamenikataza kutoa taarifa zozote mpaka hapo uchunguzi unaoendelea utakapokamilika,” alisema meneja huyo.
“Nikweli tukio limetokea, lakini sitosema ni tukio la aina gani njooni saa nane mchana nitawaeleza kila kitu,” alisisitiza meneja huyo.
Kwa upande wake naibu waziri wa nishati na madini akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa alifika hotelini hapo majira ya saa 5.30 usiku na kwa muda wa saa moja alikaa kibalazani akizungumza na mkewe na jamaa wengine kwa njia ya simu na baadaye aliingia chumbani kwake akiwa na lengo ya kwenda bafuni kuoga lakini kabla ya kufanya hilo alisikia katika Luninga taarifa muhimu ya uchaguzi wa urais wa Urusi akaamua kughaili kwenda kuoga na kwenda sebuleni kutazama taarifa hiyo.
Alisema akiwa sebuleni hapo wakati akitazama taarifa hiyo alikuwa pia akiandika mambo mbalimbali yaliyojili katika mkutano yake na wananchi aliyoifanya mchana katika tarafa ya matombo wilaya ya Morogoro na ndipo hapo usingizi ulipomshika.
Malima alisema kuwa alistuka majita ya saa 10.45 alfajiri na kujikuta akingali sebuleni na alipoingia chumbani alikuta dirisha la chmba hicho likiwa wazi na pazia likiwa limesogezwa na kukuta vitu kadhaa vimeibiwa ndipo alipolazimika kutoa taarifa kwa uongozi wa hoteli ya Nashera
Hata hivyo naibu waziri huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa bado tukio hilo linatatanisha kwa vile mtu aliyeingia ndani ya chumba chake kuiba inaonekana kama kwamba alikuwa na taarifa za kutosha juu yake kutokana na jinsi alivyofanikiwa kubenjua roki ya dilisha hilo na kisha kuingia ndani bila ya kuhofu chochote.
Naibu waziri huyo alitumia pia fursa hiyo kukanusha baadhi ya taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii ya Jambo Forum na Fecebook inayomwelezea yeye kuwa ameibiwa vitu vyote ikiwa ni pamoja na nguo zake zote na kubakia na nguo za ndani.
Alisema kuwa nguo zake hazikuibiwa isipokuwa ni suruali moja aina ya jeans na kwamba tayari jeshi la polisi mpaka kufikia majira ya saa 8.00 mchana lilikwisha fanikiwa kupatikana kwa begi moja lililokuwa limetelekezwa katika eneo la chuo cha mifugo (LITI) likiwa na baadhi ya vitu vikiwemo pasipoti mbili za kusafiria na kadi za benki.
“Aliyeniponza ni huyo kaka yangu Edward Mdoe mimi siku zote huwa nikija hapa huwa nalala vyumba vya juu sasa nilipotoa oda ya chumba niliambia chumba ninacho lala siku zote kina mtu, nikawaambia wambambie atoke lakini nilivyoambiwa yuko kaka yangu huyu nilisema basi nitalala chini,” alisema na kuongeza kuwa vingine sakata hilo lingemkuta Mdoe.
Aliongeza kuwa Polisi walikwenda kumjulisha kuwa baadhi ya vitu vyake vilikuwa vimepatikana na kwamba alitakiwa yeye kwenda kuvitambua.
0 comments:
Post a Comment