BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATANO WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MORO KWA TUHUMA ZA KUMUIBIA NAIBU WAZIRI WA KIKWETE.


Na Venance George, Morogoro

JESHI la polisi mkoani Morogoro, linawashikilia watu watano wanaotuhumiwa kumwibia naibu waziri wa nishati na madini Adamu Malima katika hoteli ya Nashera wiki iliyopita huku asilimia 90 ya vitu vilivyoibiwa vikipatikana kutoka kwa watuhumiwa hao.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Adolphina Chialo, aliwataja watu waliokamatwa kuwa ni pamoja na Maneno Juma (25), mkazi wa wa Chamwino kwa Mgulasi, Juma Athumani (23) na Ramadhani Athumani (24) wote wakazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika tukio hilo la wizi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya jeshi hilo zinasema kuwa watuhumiwa wengine, Abudalla Athumani (25) na Halima Ramadhani (37) wameunganishwa katika kesi hiyo baada ya kukutwa na mali za wizi zilizoibwa kutoka kwa waziri Malima.

Abdallah Athumani alikuwa na laptop moja aina ya Dell huku Halima Ramadhani akikamatwa na laptop moja na simu tatu ambazo alidai kufichwa nyumbani kwake na mtoto wa marehemu dada yake Ramadhan Abdallah akidai kuwa aliletewa simu hizo na rafiki yake kutoka Ulaya na kwamba alishindwa kuzihifadhi kwake kutokana na usalama mdogo.

Kamanda Chialo alisema kuwa jeshi lake lilikamata baiskeli 10 na pikipiki mbili mpya ambazo zinadaiwa kununuliwa na watuhumiwa hao kutokana na fedha walizodaiwa kuziiba kutoka kwa naibu waziri huyo na kwamba watuhumiwa walidai kuzitumia fedha zote walizozipata kutokana na tukio hilo.

Hata hivyo, taarifa zaidi zimedai kuwa kukamatwa kwa watu hao kulitokana na mzozo ulioibuka baina yao baada ya kuzurumiana kitendo ambacho kilipelekea polisi kupata taarifa hizo zilizosababisha usiku wa kuamkia juzi kutiwa mbaroni na jeshi la polisi.

Julai 8, mwaka huu Naibu Waziri wa nishati na madini Adam Kigoma Malima aliibiwa vitu mbalimbali alivyokuwa navyo katika hoteli ya Nashera ya mjini Morogoro alikokuwa amefikia mara baada ya ziara yake ya siku mbili mkoani Morogoro.

Tukio hilo ambalo limethibitishwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro, lilitokea majira ya saa 10.45 alfajiri ya kuamkia Machi 9 ambapo wahumiwa hao wanadaiwa kukata roki ya dirisha la chumba namba 125 alichokuwa naibu waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu vyenyathamani ya zaidi ya Sh23.3 milioni.

Vitu hivyo vinajumuisha laptop tatu aina ya Dell zenyethamani ya Sh5.6 milioni, vinasa sauti viwili na headphone zake zote zikiwa na thamani ya Sh1 milioni, simu tatu Nokia C6 ya Sh500, 000, Nokia E200 ya Sh250, 000 na Blackberry ya Sh5.5 milioni.

Vingine ni pete mbili za silva zenye thamani ya Sh2.5 milioni, fedha taslimu dola za kimarekani 4,000 (Sh6.5milioni), fedha za kitanzania Sh1.5 milioni, kibagalashia chenye thamani ya Sh50,000 kadi mbili za benki, mabegi matatu, moja la nguo na mengine ya kompyuta na nyaraka mbalimbali za serikali.

Hata hivyo katika tukio hilo wezi walioiba vitu hivyo hawakuweza kuiba siraha aina ya Bastola na shortgun alizokuwa nazo naibu waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: