WAZIRI WA MAENDEELEO YA MIFUGO NA UVUVI, DK DAVID MATHAYO KULIA AKIELEZEA JAMBO HUKU KATIBU WA WAFUGAJI WA ASILI KIJIJI CHA WAME-SOKOINE WILAYA YA MVOMERO MKOA WA MOROGORO AKIFUATILIA KAULI HIYO WAKATI WAZIRI HUYO ALIPOTEMBELEA KIJIJI HICHO KUSIKILIZA KERO MBALIMBALI ZINAZOWAKABILI WAFUGAJI WA WILAYA YA MVOMERO MKOANI MOROGORO.
WAZIRI WA MAENDEELEO YA MIFGO NA UVUVI, DK DAVID MATHAYO WA KWANZA KUSHOTO AKIMSIKILIZA LEKWENANI MKUU WA WAFUGAJI MKOA WA MOROGORO, NDIKIRA LOPEJO AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WAZIRI HUYO ALIPOTEMBELEA KIJIJI WAMI-SOKOINE KUSIKILIZA KERO MBALIMBALI ZINAZOWAKABILI WAFUGAJI WA WILAYA YA MVOMERO MKOANI MOROGORO.
AKINAMAMA WAFUGAJI WA JAMII YA KIMASAI KIJIJI CHA WAMI-SOKOINE WAKIWA WAMEJIKINGA NA MWAMVULI ILI WASILOWE BAADA YA KUNYESHA MVUA WAKATI WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI DK DAVID MATHYO DAVID.
HAPA NI SEHEMU YA WANAUME WA JAMII YA KIMASAI PAMOJA NA WAGENI WA WAZIRI HUYO.
SEHEMU YA AKINAMAMA WA JAMII YA KIMASAI WAKIMSIKILIZA WAZIRI HUYO.
JAMANI HAMJAMBO MMPENDEZA !.
AFISA HABARI NA MAHUSIANO WIRAZA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI, JUDITH MHINA.
Serikali kuwanyang’anya ardhi wawekezaji
Esther Mwimbula, Mvomero.
SERIKALI imeahidi kuwanyang’anya wawekezaji maeneo ya ardhi waliyochukua na kuyatelekeza bila ya kuyatumia kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji.
Akizungumza na wafugaji wa jamii ya Kimasai hivi karibuni, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo, alisema wananchi wamekosa maeneo ya kuendeshea shughuli mbalimbali za uzalishaji, baada ya eneo kubwa la ardhi kuhodhiwa na wawawekezaji walioshindwa kuiendeleza.
Dk Mathayo alisema wananchi wa wilaya za Mvomero, Kilosa za nyingine wamekuwa wakilalamika kukosa maeneo ya kulima na kufanyia ufugaji, kutokana na eneo kubwa kumilikiwa na watu wachache ambao hadi sasa wameshindwa kuyatumia.
Alisema wakati umefika kwa Serikali kutengua umiliki wa ardhi kwa wawekezaji ambao kwa kiasi kikubwa wameshindwa kutumia ardhi waliyoomba, ili kuwarudishia wananchi wanaoihitaji.
Waziri huyo alisema wawekezaji wanatakiwa kutambua kuwa maeneo wanayopewa na Serikali wanapaswa kuyaendeleza kwa shughuli za maendeleo na kuliongezea taifa kipato.
Alisema kuna wawekezaji wengi wanaohitaji maeneo ardhi ili waweze kuongeza pato la taifa, hivyo wanatakiwa kulinda na kuheshimu taratibu na sheria za nchi kulingana na mikataba yao.
Pia, Dk Mathayo alisema imebainika kuwapo Watanzania wengi ambao wanaweza kuwekeza na kusaidia kuongeza pato la taifa, hivyo haina haja ya kuwang’ang’ania walioshindwa kuyaendeleza.
0 comments:
Post a Comment