Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) Pascal Kihanga akimkabidhi zawadi na kombe nahodha Sembuse Parisi mara baada ya kumalizika kwa fainali ya ligi ya taifa ya kuwania ubingwa wa mkoa wa Morogoro na klabu ya Mkamba Rangers kuibuka mabingwa wapya 2011/2012 katika hafla iliyofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro wa kwanza kushoto ni Kaibu Katibu wa soka mkoa huo Emmanuel Kimbawala.
Wachezaji na viongozi wa klabu ya Mkamba Rangers FC ya wilayani Kilombero wakishangilia ubingwa wa mkoa wa Morogoro kwa msimu wa mwaka 2011/2012 baada ya kumalizika kwa fainali ya ligi ya taifa kuwania ubingwa wa mkoa huo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
KLABU ya soka ya Mkamba Rangers FC imetwaa ubingwa wa mkoa wa Morogoro 2011/2012 baada ya kufikia tamati kwa michezo ya fainali wa ligi ya taifa kuwania ubingwa huo dhidi ya Mpepo FC ambapo mchezo huo ndiyo uliamua bingwa wa ligi hiyo ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 katika mchezo mkali na kusisimua uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Ubingwa wa mwaka 2011/2012 uliamuliwa na kanuni ya mabao ya kufungwa ambapo klabu ya Mkamba Rangers FC ilipata faida ya sare hiyo baada ya nyavu zake kutikiswa mara mbili kutokana na kupata sare mbili na kushinda michezo miwili ikiwa imejikusanyia pointi 11 huku Mpepo FC yenyewe ikilingan na idadi ya pointi na mabao ya kufunga tofauti ikiwa imetandikwa mabao matatu hivyo kulingana kanuni ya ligi hiyo Mkamba Rangers FC wametawazwa kuwa mabingwa wapya wa mkoa huo kutokana na klabu ya Mpepo FC kuwa na idadi kubwa ya mabao ya kufungwa.
Katika mchezo huo Mpepo FC ndiyo walionza kupata bao la mapema lililofungwa na mshambuliaji, Abdallah Zungu aliyetumia vema krosi ya Shaban Togwa na kupachika bao hilo kwa kichwa akiwa eneo la hatari na kumuacha mlinda mlango wa Mkamba Rangers FC, Ally Mensa akichumpa bila mafaniko ambapo kabla ya kutinga nyavuni mpira huo uligongwa mwamba wa juu.
Mkamba Rangers FC walisawazisha bao hilo lililofungwa kiufundi na kiungo mshambuliaji, Abdallah Wilemela dakika ya 21 kwa mpira wa adhabu ndogo nje kidogo ya 18 ambapo mpira huo ulienda moja kwa moja wavuni huku golikipa wa Mpepo FC, Bembe Kanuni asijue la kufanya.
Aidha bingwa wa ligi hiyo alikabidhiwa zawadi ya kombe na fedha taslimu shilingi laki moja sanjari na pea moja ya jezi huku mshindi wa pili akimbulia zawadi ya kifuta jacho cha shilingia elfu hamsimi.
Katika ligi hiyo ilishirikisha jumla ya timu sita ambazo zilifuzu kutoka vituo viwili vya mji mdogo wa Mkamba ikiwemo Mkamba Rangers, Uhuru Rangers na The Wailes huku kituo cha Kilosa ni Mpepo FC, Kaizer Chief na Docks FC ambapo michezo ya fainali hizo zilianza kutimua vumbi februari 25 na kufikia tamati marchi 3 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
0 comments:
Post a Comment