BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BENDELA AKABIDHI KOMBE KWA NAHODHA IMAN MAPUNDA BAADA YA POLISI MORO SC KUIBUKA MSHINDI KWA KWANZA BAADA YA KUMALIZIKA KWA LIGI DARAJA LA KWANZA 9-BORA MOROGORO.


Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendela akimkabidhi kombe nahodha, Iman Mapunda baada ya klabu ya Polisi Moro SC kushika nafasi ya kwanza katika ligi daraja la kwanza hatua ya 9-Bora kwa kumaliza ikiwa na pointi 20 na kufanikiwa kucheza ligi kuu ya vodacom msimu ujao wa mwaka 2012/2013 katika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa, klabu nyingine zilizofanikiwa kucheza vodacom ni JTK Mgambao Shooting Tanga ikiwa na pointi 15 na Tanzania Prinson ya Mbeya yenye pointi 14, wa pili kutoka mkuu wa mkoa ni msimamizi wa kituo Blasio Kiondo.


MKUU wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendela amezitaka klabu tatu zilizofuzu kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa mwaka 2012/2013 kufanya maandalizi ya kutoka ili kukabiliana na mikimiki ya ligi hiyo.


Akizungumza wakati wa kukabidhi kombe kwa klabu ya Polisi Moro SC kwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora Bendelan alisema kuwa ni muhimu kwa benchi la ufundi kwa klabu hiyo kuanza maandalizi ya kutosha kwa ajili ya michezo ya ligi kuu ya Vodacom msimu ujao kwani ligi hiyo imekuwa na ushindani wa hali ya juu.“Kwanza nazipongeza klabu za Polisi Moro SC, JKT Mgambo Shooting na Tanzania Prinson kwa kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao kwa kufuzu lakini niwaeleze nitajisikia vibaya sana endapo klabu hizo zitacheza msimu mmoja kisha kushuka daraja” alisema Bendela.


Klabu hizo ambazo zimefuzu kucheza ligi kuu ya Vodacom msimu ujao ni Polisi Moro SC iliyomalizika ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora mwaka 2011/2012 ikiwa nafasi ya kwanza kwa kufikisha pointi 20, JKT Mgambo Shooting imekusanya pointi 15 na Tanzania Prinson iliyoshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 14 ambapo Mgambo Shooting na Tanzania Prinson walimaliza ligi hiyo kwa kupokea vichapo katika michezo yao ya mwisho.


Katika michezo ya kufunga panzia la ligi hiyo daraja la kwanza hatua ya tisa bora JKT Mgambo Shooting ilipokea kichapo cha bao 3-0 kutoka kwa Mbeya City FC mabao yaliyofungwa na Julius Mwalukasa dakika ya 38, Innocent Bony alifunga mabao mawili katika dakika ya 72 na 74 huku Tanzania Prinson nao walitandikwa bao 2-0 na Polisi Dar yaliweka kiamiani na Henrico Kayombo dakika ya 45 na bao la pili lilifungwa na dakika 87 na Benjamin Peter na kufanya Mgambo na Prinson kumaliza ligi hiyo kwa vichapo.


Mkuu huyo wa mkoa wa Morogoro ambaye pia ni kocha wa mchezo wa soka alitumia nafasi hiyo kutoa ushauri kwa TFF kuangalia namna ya ligi daraja la kwanza msimu wa mwaka 2012/2013 michezo ya kusaka klabu ambazo zitaingia ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013 iendeshwe kwa michezo ya nyumbani na ugenini ili kuzipunguzia mzigo kwa klabu zinazoshiriki ligi hiyo.
Bendela alisema kuwa ni vizuri kujipanga mapema kwani ligi kuu itarajia kuanza kutimua vumbi mwezi wa nane hivyo kimahesabu muda uliobakia wa miezi mitatu kwa maandalizi ni mfupi na mabadala yake benchi la ufundi na uongozi wa klabu hizo kuanza maandalizi ya kutosha.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: