BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TANZANIA PRINSON YAREJEA LIGI KUU YA VODACOM MSIMU WA MWAKA 2012/2013

 Wachezaji wa Tanzania Prinso ya Jijini Mbeya wakiwa wamembeba kocha wao mkuu Steven Matata baada ya kupata moja ya nafasi tatu za juu za kucheza ligi kuu ya vodacom Tanzania bara msimu ujao wa mwaka 2012/2013 baada ya kuitanda Rhino Rangers ya Taboara kwa bao 2-0 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
                                     
Mshambuliaji wa Tanzania Prinson, Jeremia Juma kulia akichanga mbunga kwa kumtoka mlizni wa Rhino Rngers Iddi Salum wakati wa ligi daraja la kwanza hatua ya 9-Bora katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo mchezo huo Prinson walishinda kwa bao 2-0.


KLABU ya Tanzania Prinson ya mkoani Mbeya imejea ligi kuu ya vodacom Tanzania bara msimu ujao wa mwaka 2012/2013 kwa kishindo kufuatia ushindi wake dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora baada ya kuipelekesha mchakamchaka katika mchezo mkali wa ligi daraja la kwanza hatua ya 9 bora kwa bao 2-0 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.


Vijana hao wananolewa na Kocha mkuu, Steven Matata walianza mchezo huo kwa kasi huku wakitandaza soka la uhakika na kuweza kutawala eneo la kiungo hali iliyopelekea kuzima mashambulizi ya wapinzani wao na kuwapa mwanya wa kushambulia na kujipatia mabao yao kupitia yaliyopachikwa nyavuni kwenye dakika ya 37 na dakika ya 75.


Mshambuliaji, Peter Michael ndiye aliyeanza kufungua bao la kwanza kwa njia ya mkwaju wa penalti baada ya mlinda mlango wa Rhino Rangers, Abdulkarim Mtumwa kumfanyia madhambi mshambuliaji, Shabaan Mtupa katika eneo la hatari baada ya kudaka mpira wa kona uliochongwa na, Henry Mwalugala na mwamuzi Shabaan Shata kutoka Kigoma kutoa adhabu hiyo.

Bao la pili lililowapeleka Prinson katika ligi kuu ya Vodacom msimu ujao lilipatikana katika dakika ya 75 likifungwa na Jeremiah Juma akifunga kwa shuti kali akiwa ndani ya eneo la hati kwa krosi ya Peter Michael iliyowapita walinzi wa Rhino Rangers,Issa Salum na Hussein Shaibu na mpira kumkuta mfunga aliyefunga bao hilo.

Katika mchezo huo ambao ulichezeshwa vizuri na mwamuzi wa kati, Shaaban Shata kutoka Kigoma, Tanzania Prinson waliweza kupata kona nane nne, faulo mbili, penalti moja na mabao mawili wakati Rangers ikipata kona nne, faulo tatu, kadi za njano moja na haikupata bao na kufanya kufikisha pointi 14.

Msimamo wa ligi hiyo Polisi Moro SC ndiyo inayoongoza kwa kuwa na pointi 17, JKT Mgambo Shooting pointi 15 na Tanzania Prinson pointi 14 zote zikiwa zimecheza mcihezo saba kila mmoja na kufanikiwa kupata nafasi tatu za juu za kucheza ligi kuu ya Vodacom msimu ujao wa mwaka 2012/2013.

Katika mchezo uliofanyika majira ya saa 8 mchana Transit Camp iliweza kuongeza pointi na kufikisha mbili baada ya kupata sare ya pili ya ligi hiyo dhidi ya Polisi Tabora baada ya kupata sare ya bao 1-1 katika mchezo mkali na kusismua ambao ulikuwa hauna ushindi.

Tansit Camp walianza kufungwa bao katika dakika ya 66 na mshambuliaji, Kilowoka John akifunga kwa kuunganisha vizuri pasi ya Ernest Mkandi huku Transit Camp wakisawazisha bao hilo katika dakika ya 85 kwa mkwaju wa penalti na Mohamed Ussy baada ya Kombo Abasi kuangushwa katika eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Allanus Lwena kutoa adhabu hiyo iliyozaa bao.










Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: