MSHAMBULIAJI mkongwe wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Ulimboka Mwakingwe alizimia kwa nusu saa baada ya kuona mwili wa rafiki yake ambaye alikuwa askari jeshi la polisi Shinyanga, Benedict Tabejo maarufu kwa jina la, Joseph Tabejo aliyefariki dunia ghafu April 14 kwa ajali ya pikipiki mwaka huu.
Katika ajali hiyo ambayo ilihusisha pikipiki na lori aina ya scania T315 AEB ilitokea majira ya saa mbili usiku wakati askari huyo na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Dickson kupata ajali katika barabara kuu ya Mwanza-Shinyanga eneo la Savana mkoani Shinyanga.
Akizungumza na gazeti hili katika eneo la tukio mke wa mchezaji huyo katika eneo la msiba Chamwino Manispaa ya Morogoro jana, Naile Mwakingwe alisema kuwa mume wake alizimia kwa muda wa nusu saa kufuatia kubeba jeneza na kuona sura mwili wa marehemu Benedict Tabejo wakati wakitoa kutoka ndani ya nyumba kwa ajili ya ibada ya mazishi.
Neila alisema kuwa mume baada ya kuona hali hiyo alipatwa na kiznguzungu kabla ya kudakwa na kocha Mzigila na kuanza kupepewa kwa ajili ya kumpatia hewa ya kutoka ambapo hali hiyo ilidumu kwa nusu saa ambapo alipata fahamu.
“Joseph Tabejo ni mtu wa karibu sana kwetu sisi sote Ulimboka na mimi kwani kifo chake kinatukumbusha mambo mengi sana ni historia ndefu ndani ya maisha yetu (mimi, Ulimboka na Tabejo ) mafanikio aliyopata mimi na mume wangu yamechangiwa sana na familia ya Mzee Tabejo akiwemo na yeye marehemu” alisema Naila.
Neila alisema kilichomfanya mume wake azimie ni kumbukumbu ya maisha yao ambayo waliyoishi naye marehrmu kuwa urafiki wao ulifikia kiwango cha undugu hivyo kupitia mchezo wa soka ambapo walianza wote kucheza ligi daraja tatu kwa miaka ya 1998 hadi 2000 kwa klabu mbili tofauti zilizokuwa daraja la tatu za Chui Mzumbe na Mnadani katika miaka hiyo tofauti ambapo mwaka huo huo 2000 mwanzani wote walisajiliwa na klabu ya Reli Morogoro (Kiboko ya Vigogo) na kuwa kung'ara kwa ulimboka ulichangiwa na Tabejo kutoakana ushirikiano mzuri ndani ya uwanja hata na nje ya uwanja.
Naye baba mzazi wa marehemu Marios Tabeji (61) kwa taarifa za kifo chake kimekuwa cha ghafla na familia wamepokea kwa masitiko makubwa lakini yote ni mipango ya mungu na kuwa umuhimu wake katika familia ameacha pengo kubwa licha ya kuwa ana watoto sita.
Tabejo alisema kuwa alipigiwa simu na mmoja wa viongozi wa juu wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga na kupatiwa taarifa za tukio la ajali kwanza lakini muda mchache akaelezwa tena kuwa Benedict tayari ameaga dunia mara baada ya kufikishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo wakati marehemu na mwenzake wakiwa katika doria ya kawaida katika barabara ya Mwanza-Shinyanga.
“Kwa taarifa za kifo chake Benedict nilizonazo hasa baada ya mwili wake kufanyiwa uchunguzi na madaktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga nilielezwa kuwa baada ya kupata ajali katika eneo la tukio alikuwa na jeraha ndogo tu katika goti na kuwa marehemu alivunjika mabeka yote mawili na damu ilivujia kwenye chumba cha moyo na mapafu ambapo hicho ndicho kilichosababisha kifo chake” alisema Tabejo.
Benedict Marios Tabejo maarufu kwa jina la Joseph Tabejo enzi za uhai wake amewahi kuzichezea klabu kubwa za soka za Reli ya Morogoro kwa msimu wa mwaka 2000/2003, Moro United 2004/2007, Polisi Moro Polisi 2008-2009 wakati Dododma msimu wa mwaka 2009/2010 na hadi umauti unamfikiwa alikuwa akichezea klabu ya Polisi Shinyanga kwa msimu wa mwaka 2011/.2012 ambapo marehemu ameacha mjane mmoja na watoto wawili wa kiume.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment