BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JKT MGAMBO SHOOTING YAPATA NAFASI YA KUCHEZA LIGI KUU YA VODACOM MSIMU WA 2012/2013.


Mlinzi wa Polisi Tabora, Kilowoko John kushoto akitafuta mbinu ya
kumtoka mshambuliaji wa Tanzania Prinso Peter Michael kulia wakati wa
mchezo wa ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora katika uwanja wa
jamhuri mkoani Morogoro.

Mchezaji wa Transit Camp Khalfan Pandu kushoto akichuana na mchezaji

wa JKT Mgambo Shooting John Mwakatala wakati wa ligi daraja la kwanza
hatua ya tisa bora katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro ambapo
katika mchezo huo Mgambo ilishinda bao 3-0 na kupata nafasi ya kucheza
ligi kuu ya vodacom tanzania bara msimu ujao wa mwaka 2012/2013.

TIMU ya soka ya maafande wa JKT Mgambo Shooting imeungana na wenyeji klabu ya Polisi Moro SC kupata moja za nafasi kati za tatu za juu za kucheza ligi kuu ya Vodacom msimu ujao wa mwaka 2012/2013 baada ya kufanikiwa kuilaza Transit Camp katika michezo inayoelekea ukingoni mwa ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora Tanzania bara kwa kuichapa bao 3-0 kwenye mkali uliofanyikia kwenye uwanja wa jamhuri mkaoni Morogoro.


Katika mchezo huo mshambuliaji, Juma Mwinyimvua aliweza kupachika mabao mawili pekee yake wavuni baada ya ushirikiano mzuri na wachezaji wenzake, Yassin Awadhi katika dakika ya 16 na bao lake la pili akishirikiana na Joel Noel dakika ya 37.

Mshambuliaji huyo alifunga bao la kwanza baada ya kupokea pasi katikati ya uwanja na kuambaa na mpira kisha kupiga shuti kali akiwa eneo la 18 na kutinga nyavuni huku bao la pili akifunga kwa staili hiyo hiyo kufuatia ushirikiano mzuri na safa ya ushambulia ya klabu yake wakati bao la tatu lilifungwa na Nassoro Gumbo dakika ya 90+1 na kujihakikishian ushindi huo ambao umewafanya kufikisha pointi 15.

Katika mchezo mungine uliofanyika majira ya saa 10 jioni klabu kongwe Tanzania bara vijana wa Tanzania Prinson ilifanikiwa kuifunga Polisi Tabora na kufufua matumani ya kupata moja ya nafasi iliyobakiwa ambapo mchezo huo ulikuwa na umuhimu dhidi ya timu hizo kutokana na kila mmoja kutaka kushinda ili kujiongezea pointi na kuingia kucheza ligi kuu msimu ujao kwa ushindi wa bao 3-0.
Mshambuliaji John Mtai aliweza kupachika mabao mawili wavuni huku bao la tatu likifungwa na Peter Michael katika dakika ya nne ya mchezo huo uliochezeshwa vizuri na Shabaan Shata wa Kigoma.

Matei alifumania nyavu kwa bao lake la kwanza dakika ya 32 baada ya kumzidi ujanja beki wa Polisi Tabora, Kilowoko John aliyeshindwa kuondoa hatari katika eneo la hatari kabla ya kufunga bao la pili dakika ya 53 kwa kichwa kufuatia kona iliyochingwa na Lameck Simon na kumkuta mfungaji huku mlinda mlango wa Polisi Tabora Rajab Iddy akichumpa bila mafanikio.

Baada ya kushinda mchezo huo Prinso inahitaji kufanya vizuri katika michezo yake miwili iliyosali ili kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Vodacom msimu ujao baada ya kucheza michezo sita na kujikusanyia pointi 11 huku JKT Mgambo Shooting ikiwa inaongoza kwa kuwa na pointi 15, Polisi Moro SC wakishika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 14.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: