Mwanamume aliyechaguliwa na kundi la kigaidi la Alqaeda nchini
Yemen kutekeleza njama ya kuripua ndege ya Marekani imegunduliwa ni
mfanyikazi katika shirika la kijasusi la Marekani CIA.
Marekani imesema mtu aliyetumwa na kundi hilo la kigaidi kuripua bomu katika moja ya ndege zake, ni mfanyikazi wa shirika la kijasusi la nchi hiyo na pia shirika la kijasusi la Saudi Arabia na kwamba kwa sasa ameshaondoka nchini Yemen.
Hata hivyo Mtu huyo hakutekeleza azma ya Alqaeda ya kuliripua bomu hilo ndani ya ndege ya Marekani badala yake moja kwa moja alikipeleka kifaa hicho cha mripuko kwa serikali ya Marekani hatua iliyorudisha nyuma njama hizo za kigaidi.
Kwa sasa bado shirika la upelelezi la Marekani linafanyia uchunguzi bomu hilo lakini maafisa nchini humo wanasema bomu lililopatikana lilikuwa la hali ya juu mno kuliko lile la mwaka wa 2009.
Maafisa hao wameongeza kuwa wanaamini mfumo wa usalama uliowekwa katika viwanja vya ndege nchini Marekani katika miaka ya hivi karibuni ungeweza kugundua aina ya bomu lililopatikana.
Jaribio la awali
Sasa Marekani inaamini kwamba bomu hili lililogunduliwa limetengenezwa na mtaalamu wa kutenegeneza mabomu wa kundi la Al Qaeda Ibrahim Hassan al-Asiri ama moja ya wanafunzi wake.
Hata hivyo Waziri wa ulinzi Leon Edward Panetta, amesema, Marekani inastahili kuwa chonjo dhidi ya walio na nia ya kushambulia nchi hiyo na kwamba maafisa wa usalama watafanya kila wawezalo kuilinda Marekani.
Mwandishi Amina Abubakar/AP
0 comments:
Post a Comment