BASI LA KAMPUNI YA MURO LIKIONEKANA KWA MBELE MARA BAADA YA KUTEKEA KWA MORO MEI 8 MWAKA HUU KATIKA KIJIJI CHA MASEYU KATA YA GWATA MOROGORO VIJIJINI KATIKA BARABARA KUU DAR ES SAALM-MOROGORO AMBAPO KATIKA AJALI HIYO ILITOKEA MAJIRA YA SAA 12:45 IKITOKEA MKOANI TABORA.
MOTO UKIWA UNAMALIZIKIA KUWAKA SEHEMU YA MAGURUDUMU UPANDE WA KULIA.
SEHEMU YA MAGURUDUMU YA UPANDE WA KUSHOTO INAVYOONEKANA
BASI HILI LIKIONEKANA KWA UPANDE WA NYUMA.
BASI la abiria mali ya kampuni ya Muro limeteketea kwa moto baada ya kutokea kwa hitirafu katika mfumo wa umeme wa basi hilo lililokuwa likitokea mkoani Tabora kuelekea jijini Dar es Salaam.
Ajali hiyo ilitokea Mei 8 mwaka huu majira ya saa 12:45 jioni eneo la Maseyu kata ya Gwata tarafa ya Mikese barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam na kwamba basi hilo ni lenye namba za usajili T 820 BEY Scania basi lililokuwa likiendeshwa na Mahamed Ally (42) na lilikuwa na abiria 25.
Alisema kuwa baadhi ya mizigo iliweza kuokolewa lakini mingine iliteketea kwa moto na hakuna vifo wala majeraha.
0 comments:
Post a Comment