RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKITANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI LEO MEI 04, 2012 IKULU.
PICA NA OFISI YA IKULU.
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amelisuka upya Baraza la mawaziri huku akiyaondoa baadhi ya majina ya mawaziri waliotuhumiwa kuhusika katika ufisadi, kuwahamisha wengine kutoka wizara moja hadi nyingine, kuingiza sura mpya na wengine wakipanda kutoka unaibu hadi uwaziri.
Aidha kabla ya kutaja baraza hilo jipya alisisitiza kuwa, kuanzia sasa waziri anapowajibishwa basi wataalam husika katika wizara waliosababisha kuwepo kwa ubadhilifu nao pia watawajibishwa.
Baadhi ya Mawaziri wapya ni Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba, Mbunge aliyeteuliwa mchana Saada Mkuya Salum na Janet Mbene wakiteuliwa katika nafasi ya manaibu katika wizara ya Fedha, huku Sospeter Muhongo aliyeteuliwa jana kuwa mbunge akiteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini.
Baadhi ya Mawaziri waalioachwa ni waziri wa fedha Mustafa Mkulo, Waziri wa Uchukuzi Omary Nundu, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja.
0 comments:
Post a Comment