BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UMISSETA NGAZI YA MKOA WA MOROGORO 2012 KUTAFUTA TIMU ZA KUSHIRKI MASHINDANO HAYO NGAZI YA KANDA YA MASHARIKI MKOANI PWANI

MSHAMBULIAJI WA WILAYA KILOSA KIBWANA RAMADHANI AKIPIMANA UBAVU NA MSHAMBULIAJI WA MOROGORO VIJIJINI JOHN KASHINJE WAKATI WA MASHINDANO YA UMISSETA NGAZI YA MKOA WA MOROGORO KWENYE UWANJA WA JAMHURI MKOANI HAPA AMBAPO KATIKA MCHEZO HUO ULIMALIZIKA KWA SARE YA BAO 1-1.


MASHINDANO ya umoja wa michezo kwa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) 2012 yameanza kulindima kwa michezo mbalimbali ambayo yanashirikisha wanamichezo kutoka wilaya sita zinazounda mkoa wa Morogoro Mei 29 mwaka huu katika viwanja vya ndani vya jamhuri mkoani hapa.

Katika michezo ya ufunguzi mabingwa watetezi kwa upande wa mchezo wa soka timu ya wilaya Kilombero iliweza kuanza vema mashindano hayo hasa baada ya kuitandika Manispaa bila huruma kwa bao 6-0 katika mchezo mkali ambao washindi walitawala kila idara ya mchezo huo.

Licha ya timu ya soka ya Manispaa kukubali kichapo hicho cha bao hizo 6-0 waliweza kuonyesha kandanda safi na kuvutia hasa kwa pasi zao ambazo zilikuwa zikiishia katika miguu ya walinzi wa Kilombero ama mlinda mlango kufuatia safu ya ushambuliaji yao walishindwa kutumia vizuri nafasi za wazi za kufunga mabao walizopata katika lango la wapinzani wao.

Wilaya ambazo zimeleta wanamichezo wake ni pamoja na Manispaa, Mvomero, Morogoro Vijijini, Kilombero Ulanga na Kilosa.

Katika mchezo huo mabao ya washindani yaliweza kupachikwa wavuni na washambuliaji, Abogasti Mutalemo alifunga mabao mawili huku wachezaji, Ammy Bangaseka, Iman Petrol, Thomas Hamis na Salum Ramadhani wakifunga bao moja moja na kufikisha idadi hiyo ya bao 6-0 dhidi ya Manispaa.

Timu ya wilaya ya Ulanga iliweza kuanza vibaya michezo hiyo hasa baada ya kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa vijana wa wilaya ya Kilosa wakati katika mchezo soka kwa wasichana Manispaa walifanikiwa kuilalua Kilombero kwa kuilaza bao 1-0 lililofungwa na Christina Daud akifunga baada ya kuwahi mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Kilombero Elizabert Amos.

Naye Mratibu wa mashindano hayo ngazi ya mkoa, Maxmilliam Lipingu alisema kuwa licha ya vijana kuonyesha ushindani lengo kuu ni kuchagua wachezaji kwa kila mchezo ambao wataunda vikosi imara kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kanda ya mashariki yatayoanza mara baada ya kumalizika kwa michezo ya mikoa.

Lipingu alisema kuwa katika matokeo ya michezo mingine ya ufunguzi kwa upande wa mchezo wa netiboli timu ya Manispaa waliweza kuifunga Mvomero kwa vikapu 37-3 huku wilaya ya Ulanga ikitambia Kilosa kwa kuilaza kwa idadi ya vikapu17-11.

Alitaja matokeo ya michezo mingine kuwa wilaya ya Kilombero iliibuka kidedea katika mchezo wa basketiboli kwa kuilaza Morogoro Vijijini kwa vikapu 47-45 kwa upande wa wavulana wakati mchezo wa wavu wavulana Kilombero iliitambia Manispaa kwa seti 2-0 kabla ya wasichana nao wakiwalaza Manispaa kwa seti 3-2.

Lipingu alisema kuwa katika mashindano hayo kuna jumla ya michezo saba ikiwemo soka wavulana na wasichana, netiboli kwa wasichana, riadha wavulana na wasichana kuanzia mita 100 hadi 5000, basketiboli wavulana na wasichana, wavu wavulana na wasichan na tufe ambapo michezo hiyo itakuwa kifanyika kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi 11:30 jioni kwenye viwanja hivyo vya Jamhuri mkoani hapa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: