Waziri wa uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe (mwenye mawani) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Reli Tanzania (TRA) Kipalo Kisamfu wakati waziri huyo alipofanya ziara ya kutembelea kalakana ya vichwa vya treni Morogoro kaba ya kuongea na wafanyakazi ambapo kwa sasa shirika hilo linajiendesha kwa hasara hapa nchini.
Hapa waziri akiangalia fundi akitengeneza mota za kufua umeme katika treni katika kalakana hiyo.
Waziri wa uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe (katikati) akimsikiliza Paschal Mafikiri kushoto juu ya injini ya treni iliyopo katika matengenezo katika kalakana ya vichwa vya treni Morogoro mkoani hapa kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Reli Tanzania (TRA) Kipalo Kisamfu.
Sehemu ya wafanyakazi wakimsikiliza waziri Dkt Mwakyembe wakati akiongea na wafanyakazi wa shirika la reli mkoa wa Morogoro.
Safu ya viongozi wa wizara ya Uchuguzi wakiwa na waziri wa wizara hiyo Dkt Harrison Mwakyembe wa pili kutoka kulia muda mfupi kabla ya kuongea na wafanyakazi wa shirika la reli.
Katibu wa chama cha wafanyakazi TRAWU tawi la Reli Morogoro, Selungwi Ubwa akisoma risala na mapendezo kwa shirika hilo kwa waziri wa Uchuguzi Dkt Harrison Mwakyembe katika eneo la Kalakana ya vichwa vya Treni Morogoro.
Dkt Mwakyembe akitoa majibu ya risala ya wafanyakazi shirika hilo ambapo aliahidi kuyafanyia kazi ndani ya wiki mbili, kushoro ni Mkurugenzi.
NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII DKT SEIF RASHID HODPITALI YA RUFAA MKOA WA MOROGORO
Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt Seif Rashid (katikati) akizungumza jambo na kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Morogoro, Lita Lyamua na mganga mkuu wa hospitali hiyo Dk. Jofrey Mtei wakati wa ziara ya waziri huyo alipofanya ziara ya siku moja ya kutembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt Seif Rashid kulia akimjulia hali mtoto Habib Ally (1) aliyepakatwa na mama yake mzazi wake, Herena Januari katika wodi namba tano inayolaza watoto wagonjwa wanaosumbuliwa na kuharisha na kutapika wakati waziri huyo alipofanya ziara ya siku moja ya kutembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
0 comments:
Post a Comment