BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAMLAKA YA NCHI YA CHINA WAANZA KUTUMIA SHERIA MPYA YA VYOO VYA UMMA.


Mamlaka ya Manispaa ya Beijing nchini China imetunga sheria mpya yengo la kuzuia vyoo vya umma kuwa na zaidi ya nzi wawili kwa wakati mmoja.

Sheria hiyo iliyowekwa na halmashauri ya manispaa hiyo inalenga kuhakikisha hali ya usafi katika vyoo hivyo vinavyotumiwa na jamii katika hali ya usafi wa hali ya juu.


Hata hivyo haijawekwa wazi ni hatua gani zitachukuliwa iwapo nzi watazidi watu atakutwa chooni na wakaguzi  wa halmashauri ya jiji hilo.


Sheria nyingine ni kuhakikisha vyoo vinasafishwa kila mara na matumizi ya vifaa vya kisasa na mafunzo ya kutosha kwa watu wanaovitazama vyoo hivyo.


Mwandishi wa BBC mjini Beijing alisema sheria hizi mpya ni mahsusi kusaidia watu wengi mjini humo ambao hawana vyoo majumbani mwao na wanategemea vyoo vya umma.

Bila shaka watakuwa wakitazama huko na huko kutafuta nzi wa tatu yuko wapi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: