BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MHARIRI MKUU WA GAZETI LA JAMBO LEO WILLY EDWARD AFARIKI DUNIA GHAFLA MKOANI MOROGORO.

Kaka mkubwa wa marehemu aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willie Edward Ogunde, George Ongiri Ogunde wa kwanza kulia akishirikiana na ndugu, jamaa na waandishi wa habari kubeba machela lenye mwili wa mhariri huyo baada ya kufariki dunia jana usiku (Juni 17, 2012) eneo la Fost Hill kwa kifo cha hafla nyumba kwa dada yake baada ya kudondoka chini wakati wakitoa mwili huo kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika kijiji cha cha Mgumo kilichopo wilaya ya Serengeti mkoani Musoma.
                                     
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bebdera akiaga mwili wa aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willie Edward Ogunde katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitalia ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ambapo marehemu alihudhuria semina ya wahariri na waandishi waandamizi juu ya masuala ya sensa iliyofanyika ukumbi wa Edema mkoani hapa.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bebdera kulia akisikiliza jambo kutoka kwa kaka mkubwa wa marehemu aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willie Edward Ogunde, George Ongiri Ogunde muda mfupi kabla ya kuanza safiri ya kusafirisha mwili huyo kwenda jijini Dar es Salaam. 

  
Mbunge wa Jimbo la Morogoro, Abdullazzizi Abood kulia akibadilishana mawazo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Husein Bashe wakati wakisubiri ndugu, jamaa na waandishi wa habari katika tukio la kifo cha Willy Edward  nje ya chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Watoto wa marehemu Willie Edward wakiwa ndani ya gari ndogo muda mfupi kabla ya mwili wa marehemu baba yao Willie Edward Ogunde kusafirishwa kwenda jijini Dra es Salaam ambao uliondoka majira ya saa 1:15 mchana.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: