Mwanaridha kutoka shule ya msingi Mkundi, Vedastus Gililo akimaliza mbio za mita 200 kwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kuwashinda wenzake akitumia muda wa dakika 29:73 wakati wa mashindano ya umoja wa michezo kwa shule za msingi na taaluma Tanzania (UMITASHUMTA) ngazi ya Manispaa ya Morogoro 2012 kwenye uwanja wa jamhuri mkoani.
Mwanaridha Anna Charo naye akimaliza mbio za mita 200 kwa wasichana kwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kuwashinda wenzake akitumia muda wa dakika 34:45.
MASHINDANO ya umoja wa michezo kwa shule za msingi na taaluma Tanzania (UMITASHUMTA) ngazi ya Manispaa ya Morogoro 2012 yameanza kutimua vumbi kwa kushirikisha kanda nne zinazounda Manispaa hiyo yaliyoanza jana katika uwanja wa jamhuri mkoani hapa.
Akizungumza na gazeti hili katika uwanja wa jamhuri mkoani hapa Afisa Michezo Manispaa ya Morogoro, Astaria Mwang’ombe alisema kuwa mashindano hayo yameanza kutimu vumbi kwa kushirikisha wanamichezo kutoka kanda nne zinazounda Manispaa hiyo.
Mwang’ombe alisema kuwa katika mashindano hayo yanashiriki michezo zaidi ya saba ambapo wanamichezo hao wakitoka kanda za Kaskazini, Kusini, Magharibi na Mashariki.
“mashindano haya yameanza kutimua vumbi jana kwa michezo minne, miwili ikiwa soka na miwili netiboli ambapo katika mchezo wa soka timu ya Magharibi ilishinda bao 1-0 dhidi ya Mashariki huku mchezo pili timu ya Kusini iliitandika Kaskazini kwa bao 2-1” alisema Mwang’ombe.
Aliongeza kuwa katika mchezo wa netiboli timu ya wasichana ya Mashariki ilifanikiwa kuilaza Magharibi kwa vikapu 16-2 wakati timu za Kaskazini na Kusini zilishindwa kutaambia baada ya kufungana vikapu 5-5.
Michezo ambayo wanamichezo hao kutoka kanda hizo nne wanashindana ni pamoja na mpira wa miguu wavulana na wavulana wenye mahitaji maalumu kutoka shule za Kilakala na Kiwanja cha Ndege, netoboli wasichana, mpira wa wavu wavulana na wasichana, mpira wa mikono wavulana na wasichana, riadha kuanzia mbio za mita 100 hadi 3000 kwa wavulana.
Wakati katika mbio za mita 100 hadi 1500 zikihusisha wasichana huku mbio za wavulana na wasichana wenye mahitaji maaalumu kuanzia mita 100 hadi 400, mbio za kupokezana vijiti kuaniza mita 100 hadi 400 wavulana na wasichana, ubunifu wavulana na wasichana na taaluma wavulana na wasichana.
Mwang’ombe aliongeza kuwa katika mashindano hayo ya Umitashumta 2012 yatakuwa na taaluma katika masomo ambayo wanafunzi watashindano katika hati darasa la tatu, huji yanayounganisha masomo ya hisabati, uraia na jografia darasa la nne, insha, hisabati na compasiotion kwa darasa la tano.
Mashindano hayo yanalengo la kusaka wachezaji kutoka kila timu kwa ajili ya kuunda vikosi vya michezo hiyo ambavyo vitashiriki mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa kabla ya kupata wachezi wataounda vikosi vya timu za mkoa kushiriki michezo ya kanda ya mashari Kibaha mkoani Pwani.
0 comments:
Post a Comment