BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UMITASHUMTA NGAZI YA MANISPAA YA MOROGORO.

Mwanamichezo kutoka kanda ya kusini, Victoria John (13) akirusha tufe wakati wa mashindano ya umoja wa michezo kwa shule za msingi na taaluma Tanzania (UMITASHUMTA) ngazi ya Manispaa ya Morogoro 2012 kwenye uwanja wa jamhuri mkoani hapa.

TIMU ya soka ya kanda ya mashariki imeonja ladha ya ushindi katika mashindano ya umoja wa michezo kwa shule za msingi na taaluma Tanzania (UMITASHUMTA) ngazi ya Manispaa ya Morogoro 2012 baada ya mchezo wa ufunguzi kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kanda ya maghaliribi katika mfululizo wa mashindano hayo yanyofanyika uwanja wa jamhuri mkoani hapa.



Katika mashindano hayo yanalengo la kusaka wachezaji kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Umitashumta ngazi ya mkoa wa Morogoro kwa wanamichezo kutoka kanda nne za Manispaa hiyo ikiwemo Kaskazini, Kusini, Magharibi na Mashariki.


Washambuliaji Andrew Daud na Seleman Ally ndiyo waliyoiwezesha kanda ya mashairiki kuibuka wa bao 2-0 dhidi ya kanda ya kusini Daud akifunga bao la kwanza katika dakika ya 22 huku Ally akihitimisha ushindi huo kwa kufunga bao la pili na kufanya mchezo huo kuondoka na ushindi huo.


Kanda ya magharibi ilishindwa kuendeleza ubabe wake baada ya kulazimishwa sare ya bao 2-2 na kanda ya kaskazini ambapo mabao yote mawili ya magharibi yalifungwa na Ibrahim Bakari katika dakika ya 23 na 54 huku mabao ya kanda ya kaskazini yakipachikwa na Mussa Abdallah dakika ya 26 na Frank Aloyce dakika ya 29.


Katika mchezo wa netiboli magharibi ilipokea kipigo kutoka kwa kaskazini kwa vikapu 7-3 huku kanda ya mashariki ikiitandika kanda ya kusini kwa vikapu 18-7.


Ismail Hussein kutoka kanda ya mashariki aliibuka na ushindi wa kwanza baada ya kumaliza mbio za mita 100 kwa sekunde 14:21 huku Magreth Soli wa kanda ya magharibi akishindi kwa upande wa wasichana kwa kushika nafasi ya kwanza katika mbio hizo na kumaliza kwa sekunde 15:62.


Katika mbio za 400 Janeth Kiguye alikimbia na kushika nafasi ya kwanza kwa kumaliza kwa dakika 1:14 wakati Abdallah Mohamed akiibuka na kwanza kwa kumaliza dakika 1:06, wakati mbio za mita 800, Joseph Amani kutoka kanda ya kusini alishika nafasi ya kwanza kwa kumaliza dakika 2:50 na Winifrida Joahan kanda ya kanda ya kusini akimaliza kwa dakika 2:36.


Masalu Magige (14) kutoka kanda ya kaskazini aliibuka mshindi wa kwanza katika kurusha mkuki mita 26:00 huku katika kurusha kisahani mita 16:93 na Zacharia Charles akiibuka mshindi wa kwanza katika kurusha tufe kwa futi 26:00 wakati kwa upande wa wasichana Victoria John kanda ya kaskazini akirusha kisahani kwa umbali wa mita 11:00.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: