Waziri wa Maji Profesa, Jumanne Maghembe kulia na Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood kushoto wakimsikiliza Mkurugrnzi wa idara ya majitaka na majisafi mkoa wa Morogoro John Mtaita (katikati) wakati waziri huyu alipotembelea mradi wa millenium charenges corpotation (MCC) baada ya kutembelea vyanzo vya maji vya Mwanambogo ambapo kumamilika kwa mradi huo utasaidia upatikanaji wa maji na upungufu wake katika maeneo ya Mkundi, Tungi na Kihonda mkoani hapa.
Mtaalamu Mshauri wa mradi huo, Tom Kililea kushoto na Profesa Maghembe kulia wakimsikiliza mkurugenzi wa idara hiyo John Mtaita katikati katika eneo la kituo kikuu cha kutibu maji Mafiga ambako kutaanzia kutandikwa mabomba ardhi yenye uwezo mkubwa wa kupitisha maji na kwenda kwa wananchi .
Profesa Maghembe mbele mara baada ya kupata maelezo katika eneo la kutibu maji Mafiga
Profesa Maghembe wa pili kutoka kulia akizungumza jambo katika eneo la bilaka la maji ambalo bilika hilo litapokea maji kutoka chanzo cha Mwanambongo katika ziara hiyo.
Profesa Maghembe akiangalia mota mojawapo zinazosaidia kusukuma mitambo na kupeleka maji maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro.
Profesa Maghembe akiteta jambo na mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood katika kituo cha kusambaza maji cha Tumbaku.
0 comments:
Post a Comment