Treni ikiteketea kwa moto wakati juhudu za uokozi zikiendelea
WATU zaidi ya 30 wameuawa Kusini mwa India katika mji wa Chennai kwa
kuteketea kwa moto baada ya gari moshi walilokuwa wanasafiria kuwaka
moto Julai 30, 2012.
Mkasa huo umetokea Jumatatu asubuhi wakati gari moshi hilo
lilipokuwa linatokea mjini New Delhi na kusababisha abiria wengine
zaidi ya 20 kujeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.
Maafisa wa uokoaji kwa sasa wanaendelea na shughuli za
kuwatafuta watu zaidi ambao huenda wamekwama ndani ya gari moshi hilo
huku idadi ya wafu ikitarajiwa kuongezeka.
Walioshuhudia mkasa huo wanasema, waliona gari moshi hilo likiwaka
moto likiwa safarini, mkasa ambao umeleta kumbukumbuku ya ajali
nyingine ya gari moshi iliyotokea mwezi Mei mwaka huu baada ya magari
Moshi kugongana na kusababisha zaidi ya watu 20 kuuawa.
Taasisi inayoshughulika na maswala ya ajali za terni nchini humo
inasema kuwa tangu mwaka 2009, watu 25,705 wameuawa kutokana na ajali
za gari moshi.
Ajali mbaya zaidi ya gari moshi iliyowahi kuikumba nchi hiyo ilikuwa
mwaka 1981 ambapo watu 800 waliuawa baada ya gari moshi la abiria
kuzama katika mto katika jimbo la Bihar.
Serikali ya India inasema iko katika harakati za kuimarisha sekta ya safari za reli kwa kuimarisha usalama wa magari moshi.
0 comments:
Post a Comment