Mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi wa pili kutoka kulia akiwa na viongozi mbalimba wa mkoa wa Morogoro wakiangalia shughuli ya mazishi ya raia 22 wa Ethiopia katika makaburi ya Kola mkoani hapa.
Baadhi wa wakazi wa Morogoro wakiendelea na kazi ya kushiriki mazishi hayo.
Hapa mwili wa mmoja wa raia hao ukiwa katika hatua za kuzika katika kaburi.
Wananchi hao wakishuka mwili wa mmoja wa raia hao tayari kwa kuzika.
Malori ya Manispaa ya Morogoro ambayo yamebeba miili ya raia hao yakiwasiri katika eneo la Kola kwa ajili ya shughuli ya kuzika.
Askari Polisi Manispaa ya Morogoro akikagua makaburi muda mfupi kabla ya kazi ya kuzika miili hiyo.
MIILI 22 ya raia wa Ethiopia
waliofariki dunia katika msitu wa Chitego wilaya ya Kondoa mkoa wa
Dodoma kwa kukosa hewa wakati wakisafirishwa kwa lori kwenda nchini
Malawi imezikwa jana katika makabuli ya Kola manispaa ya Morogoro na
mazishi hayo kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Said Amanzi
pamoja na viongozi mbalimbali wa dini.
Akizungumza
mara
baada ya mazishi hayo Mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi alisema
shughuli ya mazishi ya raia hao wa Ethiopia imefanya baada ya kukamilika
kwa uchunguzi wa kidaktari pamoja na vinasaba DNA na kwamba imezingatia
taratibu zote za
mazishi ya binadamu ikiwa ni pamoja na kuwahusisha viongozi wa dini kuu
mbili ambao waliendesha idaba ya mazishi kwa kuongozwa na imani zao.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema kuwa kabla ya kufanyika kwa mazishi hayo
Serikali ya Wilaya na Mkoa iliwasiliana na viongozi wa dini ya Kiislamu
ambao waliwakilishwa na kaimu shekhe mkuu wa mkoa wa Morogoro Ally Omary
na kwa upande wa dini ya kikristo na Katekista Mkuu wa Parokia ya Mt.
Patrice Kanisa kuu Morogoro Corbinian Banzi
ambao kwa pamoja waliwaongoza wananchi pamoja na viongozi mbalimbali
katika ibada ya mazishi hayo.
Amanzi
alisema
kuwa baada ya idara ya uhamiaji kukamilisha taratibu zao ikiwa ni
pamoja na kuwasiliana na ubalozi wa Ethiopia uchunguzi wa miili hiyo
ulifanywa Juni 28 na jopo la madaktari
likiongozwa na Dkt. Makata na baada ya uchunguzi
ilibainika walipoteza maisha kwa kukosa hewa safi (oksijeni) wakati
wakisafirishwa na roli.
Wakati
miili hiyo ilipokuwa chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya rufaa
ya mkoa wa Morogoro miili 16 kati ya 22 ya raia hao ilitambuliwa kwa
majina wakati sita ilishindwa
kutambuliwa na hivyo miili hiyo ilikuchukuliwa damu kwa
ajili kuchukua vipimo vya DNA ili ndugu wa marehemu hao waweza
kuwatambua.
Aidha
Amanzi
alisema kuwa tukio hilo ni kubwa kutokea hapa nchini na kutoa wito
kwa vyombo vya dola ikiwemo idara ya uhamiaji kuwa waangalifu zaidi
katika maeneo ya mipaka ya nchi ambao inadaiwa ndiko wanakoingilia
sambamba na kuwabaini watu
wanaosafirisha raia wa nchi za nje.
Waliotambuliwa
kwa majina ni pamoja na Jarafa Hailemaria, Agafa Sawicho, Makatosi Kibam, Lire
Aba, Teasati Sebeto, Handibo Balalio, Gilima Dandau, Ashnafu Hanifu, Elias
Kachoke, Sabato Iribeto, Yomanes Bachore, Solomon Asham na Adese Bukori wote
wakitoka katika mkoa wa Hadia nchini Ethiopia.
Wengine waliotambuliwa
kwa jina moja ni Abraham na Samira ambao wanatoka mkoa wa Hadia wakati Buligeta
akitoka mkoa wa Kambata.
0 comments:
Post a Comment